UVCCM YAZIDI KUJIMARISHA
Kaimu Katibu Mkuu uvccm Taifa SHAKA HAMDU SHAKA akikabidhi kadi kwa wanachama wapya wilaya ya Mwanga Kaimu katibu mkuu UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akifungua shina la wakereketwa wa CCM katika kijiji cha Mtalang'a kikundi cha ngoma kutoka katika kabila la kichaga kikitumbuiza wakati wa kaimu katibu mkuu wa UVCCM akiwasili wilayani Mwanga Na Woinde Shizza, Mwanga Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umewataka wananchi wa mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania kukataa na kuzikwepa siasa za uzawa na ukanda kwasababu ubaguzi ni dhambi isiyosamehewa na mungu. Wametakiwa kutambua kuwa ubaguzi ni zaidi ya laana ambayo ikiemea na kujengeka katika jamii kuiondosha kwake ni kazi ngumu na kwamba kafara yake lazima maisha ya watu yapotee au damu imwagike. Hayo yameelezwa leo na Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu shaka wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika kijiji cha Mtalang'a kata ya Mwanga mkoani hapa. Shaka alisema ni aibu binadamu aliyestaarabika, kupata elimu akawa...