Machapisho

Aspirini Tumaini jipya kwa wagonjwa wa saratani

Picha
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza, wengi tumekuwa tukiichukulia dawa ya aspirini kama dawa ya hadhi ya chini, hatufahamu kuwa ina uwezo mkubwa wa kitiba mwilini ikiwamo kuzuia magonjwa ya moyo na kiharusi. Mamilioni ya watu duniani humeza vidonge hivyo kupunguza hatari ya kufa kwa magonjwa ya moyo na kiharusi baada ya kupewa ushauri na wataalamu wa afya. Tafiti mpya zinaleta tumaini jipya kwa wagonjwa wa saratani, matokeo chanya ya tafiti mbalimbali duniani yanaleta ushahidi mpya ya uwezekano wa dawa hii kuzuia na kutibu saratani mbalimbali. Kwa mujibu wa taasisi za dawa za ndani na nje ya nchi, dawa hii ambayo ni moja ya dawa zisizo na gharama ni salama kwa matumizi ya binadamu. Taarifa za kitabibu na kifamasia zinaonyesha kuwa faida ya kutumia dawa hii ni kubwa kuliko madhara machache yanayojitokeza, ndiyo maana haikuwahi kuzuiwa kwa matumizi ya binadamu. Miaka ya nyuma dawa hii ilikuwa mwokozi wa kila siku kwa watu wengi, hasa waliopatwa na maumivu ya mwili na homa. B...

Wakazi laki 2 wilayani Musoma hatarini kiafya

Picha
Wakazi zaidi ya laki 2 katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara wanatumia maji yenye vimelea vya magonjwa ya kuambukiza,jambo linalofanya kukumbwa na magonjwa ya kuambukiza mara kwa mara. Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma Dkt. Khalfan Haule wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko hasa ugonjwa wa kipindupindu,kutokana na wananchi kutumia maji ya ziwa Viktoria. Kwa mujibu wa sampuli 14 zilizopimwa za maji wanayotumia wakazi hao zilionekana maji hayo kuchanganyika na kinyesi cha binadamu jambo linalochochea ugonjwa wa kipindupindu kushamiri eneo hilo. Mkurugenzi huyo amesema kati ya wagonjwa 10 wanaougua kipindupindu 7 ni wavuvi jambo linaloashiria ukweli wa sampuli zilizopimwa ambapo tangu ugonjwa huo umeingia watu 789 wameambukizwa na 37 kupoteza maisha. Aidha Mkuu wa wilaya ya Musoma ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Zelote Steven amesema ni wakati wa kuacha siasa kwa watendaji kuelekea maeneo hus...

Unataka kuacha sigara ?..... fuata njia zifuatazo

Je, unataka kuacha kuvuta sigara? Sawa, nakubaliana na wewe lakini unajua kwa nini unataka kuacha tabia hiyo ambayo umeizoea kwa muda mrefu?. Kwa sababu haitoshi tu utake kuacha kuvuta sigara bila kuwa na sababu muhimu inayokusukuma uache suala hilo. Kwa hivyo kwanza anza kujiuliza kwa nini unataka kuacha sigara. Kujua sababu kutakusaidia katika kutekeleza lengo lako vyema. Je, unaacha sigara kwa kuwa unataka kuilinda familia yako isipate madhara ya sigara unazovuta? Je, unataka kuacha sigara kwa kuwa umeogopa kupata kensa ya kifua? Au je, ungependa kuonekana kijana zaidi? Tafuta sababu muhimu ambayo itaizidi hamu yako ya kuvuta sigara. Jua kuwa ni jambo gumu kuacha tabia uliyoizoea kwa muda mrefu mara moja. Haitowezekana utupe kipande chako cha sigara yako mara moja na kutangaza kuwa umeacha kuvuta. Suala hilo ni gumu kwani asilimia 95 ya watu wanaojaribu kuacha sigara kwa mtindo huo hushindwa, inabidi upate ushauri na tiba mbadala ili kukusaidia kuacha kuvuta sigara, hii ni kwa sab...

Kwanini Sisi Wanawake/Wasichana Wanene na Wenye Makalio Hatupati Waume wa Kutuoa?

Picha
Nimefanya uchunguzi yakinifu na nikajiridhisha kwa 95% kuwa sie wanawake wanene na wenye makalio makubwa huwa ni ngumu sana kuolewa, kwa nini? 1. Tunaongoza kwa kuwa vimada kwa waliooa, lakini sisi hatuolewi: (a) Miili yetu imepitwa na wakati? (b) Labda wanadhani tutashindwa mechi?. 2. Tufanyaje ili nasi tupate wanaume wa kutuoa? (a) Tuifanyie miili yetu diet/tujikondeshe ili tuwe wembamba, (b)Tuanze kuwatongoza wanaume.

Breaking News:Walimu Wote wa Shule za Sekondari na Msingi Jijini Dar Kuanza Kusafiri Kwa Daladala Bure

Picha
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda kwa kushirikiana na wamiliki wa vyombo vya usafiri Dar es salaam wametangaza kuanzisha mpango wa kuwasaidia Walimu wa Shule za Serikali kwa kuwapatia huduma za usafiri bure katika daladala. Akieleza mbele ya waandishi wa habari Makonda amesema ‘Nilianza kuongea na vyama vya usafirishaji kisha kujenga hoja dhidi ya changamoto za Walimu wetu, na nikawaomba viongozi hao tuonane kulijadili hili na kisha tukafika muafaka ’ ‘Na muafaka huo ningependa kuwatangazia Walimu na Watanzania, yakwamba sasa kuanzia tarehe 7/3/2016 Walimu wa Shule za msingi na wasekondari watasafiri bure kwenye vyombo vyetu vya usafiri kwa Mkoa wa Dar es salaam’ ‘Tumeweka utaratibu, Walimu watalazimika kutengenezewa vitambulisho maalum ambavyo kila Shule itatengeneza vitambulisho vyake, huku kukiwa na mambo manne ya kuzingatia ambayo ni 1. Picha ya Mwalimu husika, 2. Jina la shule 3. Namba ya Mkuu wake wa shule 4. Kuwe na sahihi ya Mkuu wa Wilay...

UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (Ovarian Cyst) (PLIZ SHARE)

Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama 'Ovarian Cyst'. Uvimbe huu hutokea kwa wanawake wa umri wowote ule na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. Lakini kwanza hebu tuelezee juu ya mayai ya mwanamke. Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto kwake. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (Uterus). Mayai haya ya mwanamke huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama 'Ovum' na mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (Ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni. Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, masaa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya 'Luteinizing Hormone' kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa katika kila 'Ovari' na hii...

Maajabu ya dunia jamani! Huyu jamaa anatoka nchini Nepal na anaonyesha ubabe wa kujifunika na mamilioni ya nyuki

Picha
Oh jamani! Huyu jamaa anatoka nchini Nepal na anaonyesha ubabe wa kujifunika na mamilioni ya nyuki kwa mwili wake bila hata ya mmoja kumuuma. Surya Prasad Lamichhane, mwenye umri wa miaka 34, amekuwa akifuga nyuki kwa miaka 9 na anawachukulia kama marafiki zake wa karibu.