Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2019

Wanne Watia Mbaroni Jijini Arusha kwa Kutengeneza Fedha Bandia

Picha
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limewakamata watuhumiwa sita kwa makosa mbalimbali. Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ramadhani Ng'anzi amesema jana Ijumaa Januari 18, 2019 kuwa watuhumiwa wanne ambao hakuwataja majina yao kwa sababu za kipelelezi wanajihusisha na utengenezaji wa fedha bandia. Amesema mtuhumiwa wa kwanza alikutwa na noti bandia za dola za Marekani  zenye thamani ya dola 500 (zaidi ya Sh 1.1 milioni). "Huyu mtuhumiwa wa kwanza aliwapeleka askari wetu nyumbani kwake eneo la Daraja Mbili ambako zilikutwa fedha bandia za mataifa mbalimbali," alisema Ng'anzi Fedha hizo ni dola za Marekani, fedha za Umoja wa Ulaya (Euro), Kenya, Malawi, Zambia, Rwanda na Sudan. Alisema watuhumiwa wanashikiliwa kwa ajili ya mahojiano na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani. Katika tukio jingine, Ng'anzi amesema kuwa watuhumiwa wengine wawili ambao ni Kennedy Mbilinyi na Richard Loishiye wamekamatwa kwa kuiba gari aina Harrier lenye namba za usaili T 241 DKC n...

Kigwangalla Aivunja Bodi ya Utalii (TTB)

Picha
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amevunja bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuanzia jana Ijumaa na kutoa miezi mitatu kwa menejimenti kujirekebisha kinyume na hapo ataifumua. Waziri huyo ametangaza kuunda bodi mpya ya wakurugenzi ambayo itakuwa na wajumbe vijana watakaokwenda na kasi katika kazi hiyo ya kutangaza vivutio. Dk Kigwangalla amefikia uamuzi huo kwa kile alichoeleza kuwa TTB imeshindwa kutekeleza maelekezo yake yenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii. Akitoa uamuzi huo jana Ijumaa Januari 18, 2019 mbele ya waandishi wa habari Dk Kigwangalla ameeleza kutotangazwa kwa vivutio vya utalii kunaifanya Serikali inyooshewe kidole na kuonekana haifanyi kazi. Amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja ametoa maelekezo zaidi ya 15 lakini hayajafanyiwa kazi jambo linalosababisha yeye kutukanwa. “Serikali ikitukanwa kwenye sekta ya maliasili na utalii maana yake natukanwa mimi naonekana sitoshi kwenye nafasi hii, “ amesema Dk Kigwangalla. Miongon...

Rais Magufuli: Changamoto Zilizopo Sasa Zisipotatuliwa, Sidhani Kama Ajaye Atazitatua

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema hana uhakika endapo mrithi wake ataweza kutekeleza mambo anayoyafanya katika uongozi huu wa awamu ya tano.   Magufuli ameyasema hayo jana  Ijumaa Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Alisema katika safari ya kutatua changamoto anakutana na magumu mengi na ndiyo maana amekuwa akihitaji nguvu za Mungu kutekeleza majukumu yake. “Viongozi wa dini endeleeni kuliweka Taifa hili kwenye mikono ya Mungu. Hii ni vita kama ilivyo nyingine na vita ya uchumi inahitaji maombi sana, bila maombi kazi hii haiwezi kufanyika,” alisema. “Hao wanaokaa gizani hauwezi kujua ana kisu, ana panga au ameweka nyoka mfukoni lakini huko gizani huwa wanatolewa kwa maombi, yatawapumbaza huko gizani wasitake kufanya walichokusudia.” Alisema kufanya hivyo kutawafanya viongozi wa nchi kusimamia misingi ya uadilifu na up...

Waziri Mkuu Majaliwa Akagua Eneo Itakapojengwa Hospitali Ya Uhuru Katika Kijiji Cha Maduma Wilayani Chamwino

Picha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua eneo la ujenzi wa hospitali ya Uhuru lenye ukubwa wa ekari 109 lililoko katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.  Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Maduma wilayani humo leo mchana (Ijumaa, Januari 18, 2019), Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Serikali ya kijiji hicho wa kutenga maeneo ya maendeleo ni wa kupigiwa mfano na vijiji vya maeneo mengine.  “Uamuzi wenu wa kutenga maeneo ya miradi ya maendeleo umekuwa na tija, ndiyo maana Mheshimiwa Rais Magufuli aliposema ijengwe hospitali, hamkupata shida sababu eneo tayari lilikuwepo. Ninawapongeza wazee waliojitolea maeneo yao ili kuongeza kwenye eneo la hospitali,” amesema.  Wazee waliotoa maeneo yao ni Mzee Meshack Njamasi (ekari 5.50), Mzee Jobu Malogo (ekari 3.50) na Bw. Nehemia Mwikwi (ekari 4.50). Ekari 95.5 zilizobakia, zimetolewa na Seriakli ya kijiji hicho.  Waziri Mkuu aliwataka wakazi wa wilaya ya Chamwino wasibweteke bali wajipange na kila mmoja ajipange kufanya kazi ka...

ZIJUE NDEGE MPYA ZA AIR TANZANIA

Picha

Rais Magufuli ametwaa tuzo nyingine tena

Picha
Rais Magufuli ametwaa tuzo nyingine tena ya jarida mashuhuri la Uingereza, African Leadership Magazine (ALM), akitwaa tuzo ya upande wa uongozi katika siasa na maendeleo Afrika ambapo katika eneo hilo amefuatiwa na Rais Ramaphosa wa A. Kusini. Tuzo kutolewa Sandton, S.A Feb. 22, 2019.