Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2018

DC ARUMERU AZUNGUMZA NA MADIWANI ARUSHA DC

Picha
Mkuu Wa wilaya ya Arumeru *Mh.Jerry Muro* amewataka madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Arusha Dc kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza kiwango cha ukusanyaji katika halmashauri hiyo. *Dc Muro* ameyasema hayo hii leo katika baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Arusha ambapo amesema kuwa vipo vyanzo vingi vya mapato ambayo halmashauri hiyo inaweza kukusanya na kufika kiasi cha shilingi *billion kumi.* Licha ya kutoa agizo hilo akalazimik kutoa tahadhari ya kutolipwa posho pamoja na kuvunjwa kwa baraza la madiwani kutokana na wao kushindwa kukusanya mapato Mara baada ya kutoa agizo kwa baraza hilo La madiwani mwenyekiti wa halmashauri hiyo ndugu *Noah Lembris* amemsisitizia Mkuu wa Wilaya kuwa watazidi kufuata sheria zaidi ili kufikia maendeleo ya wananchi pamoja. Katika kikao hicho cha baraza la madiwani kimejadili pia changamoto mbalimbali ikiwemo miradi ya maji iliyokwama kwa muda mrefu ambapo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo *Dr Wilson Charles Mahe...

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI AFRIKA(OATUU) LAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA VITA DHIDI YA UFISADI NCHINI

Picha
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Afrika**(OATUU**) lililokutana mjini Dar es Salaam,Tanzania kwa mkutano wa siku limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli kwa mapambano ya dhati juu ya vitendo vya Rushwa na Ufisadi. Akisoma maazimio ya kikao hicho Katibu Mkuu wa *OATUU* *Cde Arzeki Mezhoud* amesema kwamba Tanzania ni kati ya nchi chache za mfano wa kuigwa katika mapambano dhidi ya Rushwa Afrika na Rais Magufuli ni kielelezo wa Kiongozi anayechukia Rushwa kwa Vitendo na kwamba *OAATU* inamuunga mkono katika jitihada hizi na asijione yupo peke yake katika vita hii kubwa. Akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) *Mh Anthony Mavunde* kupokea maazimio hayo ya *OATUU* kwa niaba ya Serikali,Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania *(TUCTA)* Cde Tumaini Nyamuhokya amesema TUCTA inaunga mkono jitihada za serikali kupambana na Rushwa na muda wote itashirikiana na serikali katika mapambano hayo. Ai...

Makampuni yanayoajiri Vikongwe, kutoa mishahara midogo Kikaangoni

Picha
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ametoa mwezi mmoja kwa Makapuni binafsi ya Ulinzi kuhakikisha yanarekebisha mfumo wao wa kuajiri pamoja na utoaji wa mishahara kabla ya Wizara yake haijaanza kuyahakiki makampuni hayo. Lugola amesema baadhi ya Makampuni hayo yameajiri wazee wasiojiweza ambao muda wote wanalala na wanasabaisha uhalifu kuendelea kwa kasi, wakati vijana wapo wengi wenye nguvu zao wanaweza wakazifanya kazi hizo kwa umakini zaidi, na pia tatizo lingine wanalipwa mishahara midogo hali hiyo inawafanya pia wajiingize katika uhalifu. Akizungumza na mamia ya wananchi mjini Bunda, mkoani Mara katika mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya zamani mjini hapo, Waziri Lugola alisema, Serikali ya awamu ya tano kamwe haitataka uzembe, hivyo makampuni hayo yanayovunja utaratibu huo siku zao zinahesabika. Lugola aliongeza kua, licha makampuni hayo yamekua yakiwekeza nchini na pia yanasaidia kufanya doria katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya miji, lakini yapo maen...