Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2023

KISA CHA MFALUME NAJASHI & ITHIOPIA NA UISLAMU

Picha
Uhabeshi ambayo hii leo inajulikana vyema kwa jina la Ethiopia ni nchi ambayo ni mashuhuri sana kwa Waislamu. Katika makala hii tumejaribu kadiri ya uwezo wetu kubainisha angaa kwa ufupi hali ya kihistoria, kijografia, kieneo kisiasa na kijamii ya nchi hiyo muhimu katika bara la Afrika. Katika sehemu nyingine tumejaribu pia kugusia hali ya dini tatu muhimu za Kiislamu, Kikatoliki na Kiothodoksi nchini humo. Sehemu ya mwisho ya makala hii inahusiana na hali ya hivi sasa ya Waislamu wa Ethiopia na pia uhusiano wa kiuchumi wa Iran na nchi hiyo.Maneno muhimu: Uhabeshi, Ethiopia, Uislamu, Ukristo, hajiri, jiografia, hali ya kihistoria na kisiasa, Italia, Haile Selassie, utawala wa kifalme na uhusiano wa kiuchumi. Uhabeshi inafahamika vyema kwa Waislamu kutokana na kuwa ndilo lililokuwa kimbilio la kwanza la maswahaba mashuhuri wa Mtume Mtukufu (SAW) mwanzoni mwa kudhihiri Uislamu. Kabla ya Uislamu kuenea huko Bara Arabu kundi la kwanza kabisa la Waislamu lilihajiri na kuhamia Uhabeshi kutok...