Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2022

HAPPY BIRTHDAY KARIM & RAHMU

Picha
Enyi wanangu!  Shikeni Swalah na amrisheni mema na katazeni  maovu na SUBIRIN kwa yanayo kupateni. Haya ni katika mambo ya kuzingatia sana WANANGU. Happy birthday KARIM & RAHMU  

Vita vya Badr: Chanzo na sababu za vita vya Badr

Picha
  Sura Ya 30: Vita Vya Badr Vita vya Badr: Chanzo na sababu za vita vya Badr Vita vya Badri. - Vilikuwa ndio vita vya kwanza vya jihad vilivyopiganwa siku ya Ijumaa mwezi 17 Ramadhani, mwaka wa 2 A.H (624 A.D) katika bonde la Badri. - Chanzo cha vita ni kuwa mtume (s.a.w) alikusudia kuuzuia msafara wa Maquraish wa Makkah uliotokea Syria (Sham) uliosheheni bidhaa zenye thamani ya dinar 50,000 kwa ajili ya maandalizi ya kuupiga vita Uislamu na Waislamu. - Mtume (s.a.w) alikuwa na askari 313, ngamia 70 na farasi 2 tu na Makafiri wa Kiquraish wakiwa askari 1000 waliojizatiti kivita, ngamia 700 na farasi 300. - Waislamu walipata ushindi kwa waliuawa Maqurish 70 wengi wao wakiwa vigogo wa Makkah na waislamu 14 tu waliuawa. Rejea Qur’an (3:123-124), (8:9-11), (54:45), (8:65), (8:17) na (8:48). Mafunzo kutokana na Vita vya Badri. 1.Ushindi wa waislamu katika vita unatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na sio kutokana na ubora wa silaha na wingi wa askari. Rejea Qur’an (3:123-124), (8:42-45). 2.T...