SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 12 Machi 2016

T media news

LADIES: Hizi ni Dalili 11 Mpenzi Wako Anataka Akufanye Uwe Mke Wake...Soma Hapa


Ukiotea story kwenye vikao vya wanawake, utasikia wakisema wanaume wanaooa siku hizi wamekuwa wachache. Kwamba wengi tunapenda kuwachezea tu. Lakini wapo wanaume ambao wanataka kutulia na mwanamke mmoja na kumfanya awe mke wake. Sasa utajuaje kuwa boyfriend wako anakupenda kiasi cha kutaka uwe mke wake?

1. Huweka mipango ya baadaye

Anapoanza kuzungumza mipango yake ya baadaye, ni ishara kuwa angependa ajue mtazamo wako na mtazamo wako una uzito kwake.

2. Unaalikwa kwenye kila tukio

Unakuwa mtu wa pili kwenye kila matukio muhimu. Hii inamaanisha kuwa anakuona una umuhimu kwenye maisha yake. Anataka kukutambulisha kwa familia yake na kukufanya ujisikie kuwa na wewe ni sehemu yake.

3. Yuko Makini

Kama mpenzi wako anazingatia muda, ni lazima anakukubali sana. Pindi mwanaume anapokuwa kwenye uhusiano serious, atahakikisha kuwa mwanamke wake hamsubiri. Atahakikisha unajua kama atachelewa na hatokuchomesha mahindi.

4. Kuna ongezeko la ukaribu

Itaonekana kama mlipoanza kuwa pamoja. Mwanaume wako atakuwa karibu zaidi, kukushika mkono wakati unapika au kutumia muda kukufanyia massage wakati ukifanya kazi.

5. Anakumisi

6. Anakuona wewe pekee

Hawezi kukufanya ujisikie wivu kwa kuonesha kutamani wasichana wengine hata kama mkiwa sehemu yenye watu wengi

7. Anataka muishi pamoja

8. Hufunguka mambo mengi kwako

9. Hakimbii unapokuwa kwenye wakati mgumu

10. Hakuchoki

11. Anasema kuwa anataka kukuoa