NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU.
Nunua ukwaju wako, ukwaju unapatikana kwa wingi sana masokoni na kwenye supermarkets
Andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu
Ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe
Weka sukari kwa kiasi unachopendelea pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa.
FAIDA YA JUISI YA UKWAJU.
Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
Husaidia kurahisisha choo (laxative)
Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye
vidonda
Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)