Machapisho

PUNGUZA UZITO BILA GHARAMA KUBWA

Picha
WAKATI MWINGINE JUICE YA UKWAJU NZITO INAWEZA KUKUTOA HUKO USIKOPENDA KUNAKOKUFANYA UKOSE RAHA.... MAHITAJI YAKE NI KAMA IFUATAVYO 1- Ukwaju robo kilo uliomenywa 2- Limao moja la wastani 3- Maji lita moja 4- Rojo la tende nusu kikombe Au asali vijiko vitatu JINSI YA KUANDAA Ni rahisi sana chukua sufuria yako weka ukwaju na maji kisha bandika jikoni uchemke dk 15-20 kusaidia kulainika haraka. Koroga wakati ukiwa unachemka ili utoke vizuri. Baada ya Hapo Ipua Subiri upoe kisha utoe mbegu za ukwaju na uchuje... Kamulia limao lako kisha weka Asali Au tende kama nilivyoelekeza koroga na uandae tayari kwa kunywa... Ukiishakunywa hii kitu pumzika tu home Usije pata shida safarini huko...maana unatakiwa kuinywa NZITO hivyohivyo ili ifanye kazi vizuri... Kwa maelezo Wasiliana na Doctor Seifu.

🩺 UTUNZAJI MAALUM KATIKA UJAUZITO: MWONGOZO KAMILI KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO|T MEDIA NEWS

Picha
📘 UTANGULIZI Katika sehemu ya kwanza ya moduli ya Utunzaji katika Ujauzito, ulijifunza kuhusu muundo wa mfumo wa uzazi wa mwanadamu, jinsi ujauzito unavyoanza na hatua zake, pamoja na mabadiliko yanayotokea mwilini mwa mama. Pia ulipata uelewa wa awali kuhusu maendeleo ya mimba na namna ya kutambua matatizo madogo yanayoweza kujitokeza. Sasa, katika sehemu hii ya pili, utajifunza kuhusu utunzaji maalum katika ujauzito—mbinu ya kisasa inayolenga kumpa mama mjamzito huduma bora, salama na yenye ufanisi zaidi. Utunzaji huu unasisitiza huduma binafsi kulingana na hali ya kila mama, badala ya kufuata mfumo wa jumla kwa wote. 🎯 MALENGO YA SOMO Baada ya kujifunza mada hii, utaweza: Kufafanua dhana muhimu zinazohusiana na utunzaji maalum katika ujauzito Kueleza tofauti kati ya utunzaji wa kitamaduni na utunzaji maalum Kuelewa ratiba na malengo ya ziara za kliniki wakati wa ujauzito Kutoa ushauri sahihi kwa mama kuhusu maandalizi ya kujifungua Kutambua dalili za hatari na kuchukua hatua ...

IJUE HISTORIA YA KABILA LA WAKURYA|T MEDIA NEWS

Picha
Abakuria (au Wakurya) ni kabila la watu wanaoishi katika wilaya za Rorya, Tarime na Serengeti kwenye mkoa wa Mara, kaskazini mwa Tanzania, na katika wilaya za magharibi na mashariki mwa Mkoa wa Nyanza katika sehemu ya kusini mashariki ya Kenya. Mnamo mwaka 2005, idadi ya Abakuria ilikadiriwa kuwa 690,000, ikiwa ni 430,000 wanaoishi nchini Tanzania na 260,000 nchini Kenya. Lugha yao ni Kikuria. Abakuria ni wakulima na wafugaji, huku Abakuria wa nchini Kenya wakiegemea sana kwa kilimo nao wa nchini Tanzania wakiegemea sana ufugaji. Kilimo cha asili walikuwa wanalima ulezi mtama na viazi tu kwa ajili ya kutengeneza Togwa (obosara) na Pombe. Mazao mengine yalianza kulimwa miaka ya 1900  baada ya wajerumani kuhimiza kilimo. Wakurya hawapendi kutawaliwa wala kuonewa hivyo walikuwa na saiga lika ya vijana kwa ajili ya ulinzi na usalama hivyo utumwa haukuwaathiri sana. Ila kwa kupenda kwao vita walijiunga sana na jeshi K.A.R (King African Rifle) kupigana vita ya kwanza na ya pili n...

💔 Siri Nzito Ndani ya Hoteli: Kilio, Aibu na Tukio Lisilosahaulika Maishani | T MEDIA NEWS

Picha
Simu yangu ikaanza kuita, nikapiga hatua za haraka kwenda kuipokea huku nikimgonga kidogo muhudumu begani. Kitendo cha kuinama na kuiokota suruali yangu iliyokuwa chini ili kutoa simu mfukoni, ghafla taulo langu likafunguka na kudondoka chini huku muhudumu akibaki ananishangaa. ENDELEA Nilibaki nimeshika butwaa, akili yangu ikiwa imechanganyikiwa kwa sekunde chache. Sikujua nianze wapi—kuokota taulo au kupokea simu. Aibu ilinipanda ghafla, lakini simu iliendelea kuita bila huruma. Muhudumu alikuwa amesimama kama sanamu. Hakusogeza hata jicho, macho yake yakiwa yameganda kunitazama. Nilijaribu kujisitiri haraka kwa kuokota taulo, huku moyo wangu ukidunda kwa kasi isiyo ya kawaida. Hatimaye niliitoa simu mfukoni na kuona ni Rahma anayepiga. Nikapokea kwa sauti ya kawaida kadiri nilivyoweza kujizuia: “Hello baby…” “Baby, umeshaletewa chakula?” Rahma aliuliza kwa sauti ya upole. “Ndio baby,” nikajibu huku bado najisitiri kwa haraka. “Ok, mimi nimeshafika kwa bibi. Nikitaka kuja huko nitaku...

JINSI YA KUZUIA KUTAPIKA (KICHEFUCHEFU) UWAPO SAFARINI | T MEDIA NEWS

Picha
Safari ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku, iwe ni kwa ajili ya kazi, biashara au mapumziko. Hata hivyo, kwa baadhi ya watu, safari huambatana na changamoto ya kichefuchefu na kutapika, hali inayoweza kuharibu kabisa uzoefu wa safari. Katika makala hii, utajifunza kwa kina jinsi ya kuzuia kutapika safarini, sababu zake, na njia rahisi lakini zenye ufanisi za kukabiliana na hali hii. Sababu za Kutapika Ukiwa Safarini Kichefuchefu au kutapika wakati wa safari hutokana na hali inayoitwa motion sickness. Hali hii hutokea pale ubongo unapopata taarifa zinazokinzana kutoka kwa macho, masikio ya ndani (inner ear), na mwili. Baadhi ya sababu kuu ni: Kusafiri umbali mrefu bila mazoea Kusoma au kutumia simu ndani ya gari Harufu kali ndani ya chombo cha usafiri Kula kupita kiasi kabla ya safari Hali ya hewa na mtikisiko wa gari au chombo Watu ambao hawajasafiri sana mara nyingi huathirika zaidi. Njia Bora za Kuzuia Kutapika Safarini 1. Epuka Kula Kupita Kiasi Kabla ya Safari Kabla ya kuanza ...

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU|T MEDIA NEWS

Picha
Sehemu ya pili( 02) Endelea Nayo Sarah chumbani kwake aliwaza  kwa muda sana akijiuliza  kama Wangesi anasimamisha jogoo lake hakuweza kupata jibu la  moja kwa moja maana wangesi alikuwa busy sana na maisha yake Kitu ambacho marafiki wa kiume walianza kumchukua kulingana na kutoungana nao katika suala la kufuatilia wasichana miezi ilienda na mwaka ulikaribia kuisha  Mtihani wa mwisho ulifanyika wa kuhitimu ufundi wangesi alikuwa mtu wa pili kwa ufaulu mzuri wenzake wote waliokuwa wakimcheka waliangukia pua hawakuweza kufauli mtihani ule  Sarah nae hakufanikiwa kujua ukweli kwa wangesi kama yuko sawa Baada ya mitihani kuisha wangesi alielekea nyumbani kwao huku akiwa na vyeti vizuri cheti cha udereva na utengenezaji magari alijisemea hapa malengo yangu yanaelekea kutimia sana maana njia hii nitahakikisha nafanya vitu vya maana . Wangesi alivyofika nyumbani akiendelea na kazi zake na alipokuwa akilima ilikuwa ni karibia na barabara sema tu ni bar...

SIMULIZ; MTOTO WA BOSS WANGU

Picha
Mtunzi: Bikora saidy Contact: 0742754991 SEHEMU YA KWANZA ( 01) Kuna msemo usemao usilolijua litakusumbua sana na ukilijua utatuzi wake hauhitaji nguvu sana maana itakuwa vyepesi kulikwepa au kuendana nalo Hii lilidhihirika kwa kijana Wangesi mtoto wa mzee Kamau aliyejikuta akiangukia katika dimbwi la maisha magumu sana na hakujua kipi cha kufanya ili aweze kutatua hali yake maana mzee wake alianza kumdai hela yake baada ya kufeli kidato cha nne  Huko nyumbani kwao kumbuka kuna watoto wengine husoma kwa shida sana na mzazi kupata ada ya kulipia inakuwa ni changamoto sana! Wangesi alisoma kwa shida sana alikuwa ni mtu mwenye ndoto zake za kufika mbali sana alitamani kufika chuo kikuu akiamini kuwa kufika huko ndio maisha yatakuwa yamenyooka alilia sana alipokuwa akiwaona wanavyuo wakivaa joho zao Huku akitamani na yeye awe miongoni mwao  lakini hali ngumu ya maisha nyumbani kwao ilimfanya ashindwe kuendelea na shule hali ya kuwa alimaliza kidato cha nne hakufa...