Habari sanaa na michezo

Jumamosi, 7 Machi 2026

T media news

MAREKANI WAMETUMA MELI NYINGINE MIDDLE EAST


 

Meli ya kubeba ndege ya USS Gerald R. Ford (CVN-78) sasa inaelekea Mashariki ya Kati huku vita vya Marekani na Iran vikiingia wiki yake ya pili.


Pentagon ilitoa picha Ijumaa zikionyesha Ford na USS Bainbridge (DDG-96) zikipitia Mfereji wa Suez siku ya Alhamisi, meli hizo zitasaidia mapambano dhidi ya Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran ambapo hapo awali walikuwa wamelenga meli za Marekani na za kibiashara.