Mkuu wa kituo cha tafiti maalumu za michakato ya kisiasa cha Russia amesema, uvamizi wa kijeshi ulioanzishwa na Marekani na utawala wa kizayuni dhidi ya Iran unafanyika kinyume cha sheria na akabainisha: “baada ya kuanza hujuma hii tumeshuhudia kuimarika umoja wa wananchi wa Iran kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa”.
Alexi Yarushenko amesisitiza kuwa, kinyume na matarajio ya Washington, mwisho wa uchokozi huo wa kijeshi utakuwa wa kufedhehesha kwa rais wa Marekani Donald Trump.
Yarushenko amebainisha kuwa, baada ya Washington na Tel Aviv kumuua kigaidi Kiongozi wa Iran Ayatullah Khamenei, mamia ya maelfu ya wananchi wa Iran walimiminika mabarabarani kumuomboleza, na hiyo yenyewe ni ithibati ya kufeli na kugonga mwamba mpango wa shambulio la ghafla la Marekani.
Mchambuzi huyo wa Kirusi ameeleza kuwa, Wamarekani walikuwa wakidhani utawala utaanguka kwa kumuua Kiongozi wa juu kabisa wa Iran, lakini matokeo yamekuwa ni kinyume chake, ambapo jamii ya Iran imeonyesha ni jinsi gani iko imara.
