Habari sanaa na michezo

Jumamosi, 7 Machi 2026

T media news

Waziri wa ulinzi wa Saudi Arabia Khalid bin Salman amekutana na kufanya mazungumzo na mkuu wa majeshi ya Pakistan General Asim Munir


 

Katika kikao hicho viongozi hao wa juu wa ulinzi kwenye nchi zao wameyazungumzia mashambulizi ya Iran ndani ya Saudi Arabia na namna nchi hizo zinavyotakiwa kuyajibu kutokana na mkataba wa ushirikiano wa kijeshi baina ya nchi hizo 


Saudi Arabia bado ipo kwenye juhudi za kuzishawishi nchi za kiarabu ziungane kuishambulia Iran,  


Saudi Arabia na Pakistan zina mkataba wa ushirikiano wa kijeshi na kijasusi ambapo kuna kipengele kinachosema kuwa endapo nchi Moja itashambuliwa au kuingia vitani basi nchi zote zilizopo kwenye mkataba huo zinapaswa kukabiliana na vita hivyo kwa pamoja, msimamo wa Pakistan kuhusu Iran bado haujawa mkali kwani mara kadhaa Pakistan Imekuwa ikiiunga mkono Iran.


Hata hivyo uhalisia uliopo ni kuwa japokuwa Pakistan ni rafiki mkubwa sana wa Marekani ila inatambua kuwa uwepo wa Iran unafanya suala lake la nyuklia kutozungumzwa sana hivyo endapo Iran itaanguka , itakuwa ni zamu yake kuandamwa kuhusu nyuklia hasa ikizingatiwa kuwa ndio nchi pekee ya kiislamu yenye kumiliki silaha hizo.