Kipindi ambacho dunia nzima inaogopa kusema hapana mbele ya USA kuna Taifa moja huko mashariki ya kati liitwalo Iran ndio taifa pekee lenye uwezo wa kusema hapana mbele ya USA.
USA kaenda Venezuela na bila pingamizi kaondoka na mkuu wa Nchi (Rais) Kama mwizi wa kuku, baada ya hapo akapanga uongozi wake na maisha yameendelea kama vile hakuna kilichotokea.
Baada ya Venezuela akatangaza kukitaka kisiwa cha Greenland auziwe au achukue kibabe. Mmiliki wa Greenland Denmark anasubiri mbabe apite na kisiwa maisha yaendelee.
Baada ya hapo kaenda Iran, huko ndio kakutana na mtiti haamini macho yake, kafanikiwa kumuua kiongozi mkuu ila ni kosa hatosahau mpaka mwisho wa hii dunia. Kashindwa kusimika utawala wake, kashindwa kumaliza vita na sio muda atakimbia.
Akiwa bado yupo Iran katikati ya Vita Spain anaingia kwenye target zake. Mbabe kasema Spain wanakosa uongozi imara. Kauli hii ina maana nyingi anaweza amua kwenda kusimika uongozi imara kama kawaida yake.
Kabla hatujaondoka Iran, Cuba imeambiwa ijiandae maana ndio wafuatao kwenye orodha yake ya kuiharibu dunia. Cuba wanajiandaaje wote tunasubiri tuone.
China ambae ndio Target namba moja ya USA yupo kimya kama kafumaniwa chumbani kwa mwanaume mbabe, Russia tutamtetea yupo vitani ila mh naanza kutilia shaka ubabe wake.
Mwisho, Iran ni Taifa dume na imara ndio Taifa pekee lenye uwezo wa kutunisha misuri na Marekani. Hii vita America yupo na Israel huku Iran yupo mwenyewe ila mnaona mtiti, matamko hayakatiki huko Washington, mitandaoni USA inasambaza propaganda kama wehu huku Israel mitandao ikiwa inafuatiliwa habari zisitoke nje ya Israel.
