NORTHROP GRUMAN B-2 SPIRIT AU WAWEZA KUIITA BLACK GHOST. AU STEALTH BOMBER
Ni moja ya ndege za kivita zenye uwezo mkubwa zaidi duniani. Ilitengenezwa na kampuni ya Northrop Grumman kwa ajili ya Jeshi la Anga la Marekani (United States Air Force).
Hapa ni baadhi ya uwezo wake muhimu:
1. Teknolojia ya Kujificha (Stealth)
B-2 imeundwa kwa umbo maalum la flying wing linalopunguza kuonekana kwenye radar.
Inaweza kupenya anga ya adui bila kugundulika kirahisi hata katika maeneo yenye ulinzi mkali wa rada.
2 Inaweza kusafiri zaidi ya km 11,000 bila kujaza mafuta.
Ikipewa mafuta angani (air-to-air refueling) inaweza kuruka karibu sehemu yoyote duniani bila kutua.
3. Uwezo wa Kubeba Silaha
Inaweza kubeba hadi kilo 18,000+ sawa na Tani 18 na zaid za mabomu.
Ina uwezo wa kubeba:
Mabomu ya kawaida (conventional bombs)
Mabomu ya nyuklia
Mabomu ya kisasa yanayojiongoza kwa GPS (precision guided bombs).
4. Kushambulia Malengo kwa Usahihi Mkubwa
Ina mifumo ya GPS na rada za kisasa zinazoweza kulenga malengo kwa usahihi mkubwa hata usiku au katika hali mbaya ya hewa.
5.Kasi yake ni karibu km 1,010 kwa saa (subsonic speed).
6. Marekani ilitengeneza ndege hizi zikiwa 21 tu za B-2 Spirit.
Ni moja ya ndege ghali zaidi kuwahi kutengenezwa, kila moja ikiwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 2. Lakini kwa Sasa zimebakia 19 baada ya ndege moja kupata ajali na nyingine kuondolewa kwenye Matumizi kutokana na kuharibika.
7. Majukumu yake makubwa
B-2 hutumika zaidi kwa:
Mashambulizi ya kimkakati dhidi ya malengo muhimu
Huanzisha mashambulizi ya vita kwa kuvunja ulinzi wa adui
Kubeba silaha za nyuklia kama sehemu ya mkakati wa ulinzi wa Marekani.
Kwa kifupi: B-2 Spirit ni ndege inayoweza kushambulia malengo muhimu popote duniani kwa siri, umbali mrefu, na usahihi mkubwa..
Marekani hawaitimii sana ndege hii kwenye mapigano ya kawaida ya kivita ambapo ndege aina ya F ndizo hutumika mfano F.22, F.35 nakadhalika hizi ni ndege za kawaida za kivita (Fighter)
Pale inaponyanyuliwa B-2 Spirit basi Tambua shughuli ni pevu.
