Baadhi ya wananchi nchini Marekani wameanza kutoa wito kwenye mitandao ya kijamii wakimtaka mwana wa Rais Barron Trump ajiunge na jeshi na kwenda kupigana vita nchini Iran.
Wananchi hao wanasema kama kweli familia ya Donald Trump inaamini kuwa vita hivyo ni sahihi, basi mwana wake pia anapaswa kuonyesha uzalendo kwa kwenda mstari wa mbele kama vijana wengine wa Marekani wanaopelekwa vitani.
Hasira za wananchi hao zinatokana na sababu kadhaa:
Wanasema watu wenye umri mkubwa kama Donald Trump hawapelekwi mstari wa mbele vitani bali vijana wadogo pekee.
Baadhi yao wanaamini kuwa wanajeshi wa Marekani wanapelekwa kupigana vita ambavyo havina faida kubwa kwa taifa.
Wengine wanakosoa kauli ya Trump kwamba vifo vya wanajeshi ni sehemu ya kujitolea kwao walipojiunga na jeshi.
Baadhi ya Wamarekani wanasema:
"Tumechoka kuona maskini wakipigana vita na kufa kwa ajili ya wanasiasa matajiri.
