Habari sanaa na michezo

Jumamosi, 7 Machi 2026

T media news

Serikali ya Uhispania imekana kushirikiana na operesheni za kijeshi za Marekani katika Mashariki ya Kati

 

Serikali ya Uhispania imekana kushirikiana na operesheni za kijeshi za Marekani katika Mashariki ya Kati, ikipingana na maoni yaliyotolewa awali na Ikulu ya White House.


Katibu wa habari wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt alisema Uhispania ilikubali kusaidia shughuli za kijeshi za Marekani katika eneo hilo baada ya Rais Donald Trump kutishia kusitisha biashara na Madrid.


Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania José Manuel Albares alikataa dai hilo katika mahojiano na redio ya Cadena SER.


"Msimamo wa Serikali ya Uhispania kuhusu vita katika Mashariki ya Kati na mabomu nchini Iran, kuhusu matumizi ya besi zetu, haujabadilika hata kidogo,Hatutashiriki" alisema kiongozi uyo