Habari sanaa na michezo

Jumamosi, 7 Machi 2026

T media news

Mafuta ni moja ya sekta ambayo inaingiza pesa nyingi sana duniani.


 Mafuta ni moja ya sekta ambayo inaingiza pesa nyingi sana duniani, Nchi zinazochimba mafuta ni nchi zilizoendelea kutokana uchimbaji wa mafuta mfano Qatar, Dubai, Iran, Saudi Arabia, Kuwait na ile Libya ya Gaddafi


Mafuta huchimbwa ardhini kama madini mengine baada ya kuchimbwa hutoa petrol, diezel, mafuta ya taa na bitumen ambayo hutumika kutengenezea barabara kwa hiyo hakuna kitu kinachotupwa katika uchimbaji wa mafuta


Nchini Marekani Kulikuwa na bwana mmoja alikuwa anaitwa Stanley Meyer alijitokeza hadharani kutangaza gari alilobuni mwenyewe alilolipa jina la "buggy"


Akadai kuwa gari lake ameliwekea engine inayoitwa "Water Fuel Cell" ambayo inatumia maji na ikiwa na uwezo wa kutembea kilomita 150 kwa lita moja ya maji


Uvumbuzi wa gari la maji wa Meyer ulimjengea uadui na wauza mafuta wakiona kuwa Jamaa anataka kuua biashara zao kwahiyo wakafanya njama za kumuua Meyer ili kuzuia uvumbuzi wake ambao ungeua biashara ya mafuta


Meyer baada ya kuona kuwa amekoswa kuuawa katika majaribio kadhaa aliamua kusitisha uvumbuzi wake ili kunusuru maisha yake akawa anaishi maisha ya mashaka


Siku moja alienda katika mgahawa mmoja lakini ghafla hali yake ilibadilika baada kupata mlo akaanguka chini akasikika akisema "wameniwekea sumu" dakika chake Meyer akawa ameaga dunia


Mwili wake ulipelekwa hospitali kwa uchunguzi, baada ya uchunguzi majibu ya daktari yalisema kuwa Meyer alifariki kutokana na mishipa ya kichwani kupasua, Lakini watu wengi wanaamini Meyer aliuliwa baada ya kugundua gari la maji