HABARI SANAA NA MICHEZO

Jumapili, 8 Machi 2026

T media news

Iran imeanzisha mashambulizi ya balistiki


Iran imeanzisha mashambulizi ya makombora ya balistiki pamoja na ndege zisizo na rubani (drones) dhidi ya Falme za Kiarabu (UAE) na Israel. 

Mashambulizi hayo ni hatua ya kulipiza kisasi baada ya shambulizi la usiku lililosababisha moto mkubwa katika mji mkuu wa Iran, Tehran.

Milipuko ilisikika katika mji wa Tel Aviv nchini Israel, huku UAE ikitoa tahadhari ya uwezekano wa makombora. Shambulizi hilo linakuja baada ya Israel kushambulia maghala ya mafuta nchini Iran, jambo lililosababisha moto mkubwa uliotajwa kuwa kama “mto wa moto” katika mji wa Tehran.

Kutokana na mashambulizi hayo, watu wasiopungua sita wamejeruhiwa nchini Israel, na mmoja wao yuko katika hali mbaya