Habari sanaa na michezo

Jumapili, 8 Machi 2026

T media news

Iran wametoa taarifa kuwa Radar 4 za kisasa za marekani zenye uwezo wa kutambua makombora kwa masafa marefu zimeharibiwa


 Hivyo maadui zao wajiandae kwa mashambulizi ya kushtukiza bila kupata tahadhari ya ving'ora kwenye maeneo yao 


Msemaji wa Khatam Al-Anbya Air defense base ( jeshi la anga la Iran) anaeitwa Ebrahim Zolfaqari amesema..

"Radar za kisasa za mfumo wa THAAD za marekani zenye uwezo wa kugundua mashambulizi ya makombora kwa umbali mrefu sana katika maeneo ya Al-Rahba, Al-Ruwais, Al-Kharj na Al-Azraq zimelengwa na kuharibiwa ndani ya masaa 24 yaliyopita" 


"Radar hizo za mfumo wa THAAD zilikua zinatoa tahadhari ya mapema moja kwa moja kwenye mifumo ya ulinzi ya makombora ya Marekani"


"Sasa baada ya kuharibiwa kwa Radar hizo ving'ora vya tahadhari katika maeneo ya maadui vitalia pale tu kombora litakapokua tayari limelenga shabaha, mashambulizi yatakua ni ya kushtukiza hakutakua na muda wa tahadhari"


Akamaliza kwa kusema " Na ushindi unatoka kwa Mwenyezi Mungu ambae ni hakimu wa haki"


Mchana wa leo Jeshi la Iran IRGC lilituma meseji za moja kwa moja kuwaambia wananchi wa Israel wahame nchi maana makombora yanakuja na mahandaki waliyojificha hayatakua salama tena.