SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 13 Novemba 2017

T media news

Huu Ubunifu wa Roma Mkatoliki Kila Aingiapo Stejini Hautakuwa na Madhara Baadae?

Nimemfuatilia katika Shows zake karibia zote za Tigo Fiesta na kugundua kwamba mara nyingi huingia Ukumbini au pale Stejini akiwa na mienokano ya aina hii:

Kabebwa katika Wheelchair
Kakunja mkono kama amewekewa hogo
Kafunga bandeji Kichwani
Anachechemea kama Mtu aliyeumizwa
Mikono yake imefungwa nyuma
Kashika mnyororo mkubwa
Kashika Fimbo

Je hii haitokuja kuwa na madhara makubwa labda Kwake kwa siku za baadae? Na je kwa kufanya hivi anajaribu kutuma Ujumbe gani katika Jamii na kwa wale waliomteka na kumtesa hadi kumtupa Ununio mkabala na Mahaba beach? Je kama kweli Roma Mkatoliki anajambo linamtatiza moyoni na anataka kuwaambia / kuwahabarisha Watanzania na Wapenzi wake kwa ujumla basi kwanini asiitishe tu Press Conference ili atiririke na aserereke vizuri kuliko kila siku kufumbafumba kupitia Jukwaa la Tigo Fiesta?

Ushauri

Kwa aliye karibu na Roma Mkatoliki ajaribu kumsaidia Kisaikolojia kwani naona bado hayuko vizuri na kwamba pengine Yeye anaweza kudhani amemaliza Kazi ila yawezekana kabisa wabaya wake wanamtathmini na labda wanaweza wakija mara ya pili asitupwe tena Ununio na badala yake tukamuokota pembezoni mwa Fukwe zetu akiwa ndani ya Sandarusi na Jiwe juu. Afanye tu Mziki na aache masuala ya harakati kwani nina uhakika hayawezi na yatamgharimu na kuja Kujuta.

Ni Msanii mzuri sana hata Mimi namkubali na nampenda ila nahisi kama vile ama anatumika bila Yeye kujua au ana agenda fulani ambayo labda anahisi itafanakiwa japo Mimi kila nikipima kwa macho yangu ya kuona mbali zaidi naona ni kama tu anapaka rangi upepo.

Yangu ni hayo tu Wadau.

Nawasilisha.