AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“Ndio maana nikakuambia kuwa mimi ni mwalimu na ninaijua kazi yangu.Na nimesoma sana juu ya magojwa haya tuendelee…..Ungojwa wa dengue umekuja Tanzania kutokana na vimelea au mayai ya mbu hawa kuja kwa wingi kwa kutumia maji yanayo tiririka kupitia mto Naili unao ingiza maji yake katika ziwa Victori.Na baada ya Mafuriko yaliyo tokea juzi juzi Dar,Morogoro na kwengineko kumesababisha mayai ya mbu hawa kukua na kujitotolesha na kukapatikana hawa mbu ambao dawa yake ni moja tu inayoweza kuuzuia huu ungonjwa na sidhani kama munaijua?”
“Dawa gani?”
ENDELEA
“Wewe kama wewe unahisi ni dawa gani?”
“Tukuulize wewe ambaye umesema unaijua dawa ya Dengue”
“Hivi kweli wewe umesoma masomo ya Sayansi au huo unesi umeupata baada ya kufeli form four”
Swali langu likawafanya manesi kukaa kimya huku wakinitazama wasijue cha kunijibu
“Kwa akili za kawaida mtu akiwaona nyinyi manesi wawili atajua kabisa mumeishia kidato cha nne na hamkuwa mukiyasoma masomo ya Sayansi……Na mumefeli mukaamua kuja kusomea unesi.Uongo au kweli?”
Manesi wote wakakaa kimya huku wakinitazama kwa macho ya aibu aibu
“Kabla sijaendelea na na mada yangu hivi munamjua mtu anaye paswa kwenda Mirembe munapo sema?”
“Eddy baby wewe itakuwa ni malaria imekuchanganya mpenzi wangu”
“Na wewe koma malaria haiwezi kunichanganya……Hawa manesi wenu wamenidhalilisha wakiniambia mimi sina akili vizuri na hata kama ni Malaria sijawahi siku hata moja sijawahi kupatwa na ugonjwa wa kupungukiwa na akili………Musinitumbulie mimacho yenu kama mumebwana na mlango”
“Shosti kuna mgonjwa wodi ya watoto ngoja nikamuangalie”
Nesi anayefanana na Olivia Hitler alizungumza na akaanza kupiga hatua za kuuelekea mlangoni,nikamuwahi na kumshikamkono
“Hembu rudi pale kwa mwenzako huna cha mgonjwa wala cha nini kaa unisikilize”
Nesi akarudi na wote watatu wakakaa kitandani wakinisikiliza huku nesi niliye mrudisha akionekana kutetemeka kwa woga
“Atakayetoka kabla sijamaliza somo langu nitampiga boooonge la kofi mtapisho”
“Shosti unaona shunguli ya mume wako anavyo tufanyia?”
“Masikini Eddy wangu sijui amepatwa na nini?
“Nyamazeni……Dengue kama dengue dawa yake ni rahisi sana….Kwanza mtu ambaye hajapatwa na ugonjwa huu inabidi aanze kumrudia Mungu wake mapema kwa maana asisubirie ameupata ndio anakumbuka kumuomba Mungu.Pili munatakiwa kuua mazalio yote ya Mbu kama madimbwi kufyeka nyasi ndefu zilizopo karibu na makazi ya watu au kufunika vitu vyote ambavyo munajua vinaweza kuweka maji yakasimama kwa muda mrefu kama vile vifuu na kadhaliaka”
“Mmmmm kubwa hayo hadi vifuu vipo kwenye somo”
Mama Fety alazingumza huku akinitazama kisha akawageukia wezake ambao wapo kimya wakionekana kunifwatiliwa kwa umakini somo langu
“Ujinga wako ndio utakufanya ufe na dengue ninakuambia muvichome vifuu vyenu wewe unaropoka ropoka maswala ya ajabu…….Sasa tuje kwenye dawa halisi ya kutibu ugonjwa huu…..Unapaswa kunywa maji mengi ambayo yataweza kuchuja sumu iliyo jaa mwilini mwako ikiwemo bacteria wa ugonjwa huu wanao itwa ARBOVIRUS ambao watatoka kwa njia ya haja ndogo au kutokwa na jasho mwilini”
“Mwalimu nina swali?”
“Uliza”
“Hao bacteria wanaingia ingia vipi mwlinini mwa binadamu?”
“Ndio maana nikasema nyinyi manesi munaonekana hamjasoma kabisa masomo ya sayansi.Hapa si tunazungumzia huyu mbu anaye itwa AEDES ndio msambazaji wa hawa bacteria wanaosababisha Dengue sasa usicho kielewa wewe ni nini?”