MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Nikajipapasa haraka haraka kwenye mifuko yangu, ya pensi niliyo ivaa na kukuta kweli walet yangu haipo, ambayo ndani yake inapesa nyingi pamoja na vitambulisho vyangu vya kazi na bima za afya, tunazopewa wafanyakazi wa serikalini kwa ajili ya matibabu ya bure katika hospital yoyote ndani ya nchi ya Tanzania
"Asante sana dada yangu sijui nikuchukuru vipi sema nikupe nini?"
ENDELEA
"Hapana kaka yangu asante"
"Hapana jamani basi turudi nikakulipie sahani ya chipsi uliyo agizia"
"Nashukuru kaka yangu siku nyingine utanilipia"
Kabla sijazungumza simu ya yule dada ikaita akapokea ikanibidi nikae kimya, nimpe nafasi ya kuzungumza na mtu aliye mpigia
"Halow baby nakuja namalizia kufungia hizi chipsi”
“Jamani mume wangu kuna foleni kama nini"
Akamaliza kuzungumza na simu, na kukata simu
"Kaka yangu Mungu akipenda tutaonana shemeji yako ana wivu sana"
"Sawa nisalimie shemeji yangu kwa maana anafanya kazi sana"
”Kazi gani?” Dada aliuliza huku akitabasamu usoni mwake
“Kazi ya kukutunza, ndio maana ulipo ingia pale tukakukodolea macho”
"Hahaaa, mbona kawaida”
“Kwako ndio kawaida ila sisi, mmmmm”
“Usijali utapata mwenye naniliu kama langu”
"Samahani kama huto jali chukua namba yangu"
Nikamtajia namba zangu kisha akaondoka kwa mwendo wa haraka na kuniacha nimeduwaa nikiyatazama makalio yake makubwa jinsi yanavyo tingishika kama simu ya kichina yenye vibrate kali
"Mmm huku Tanga ni noma"
Nilijisemea kimoyo moya na kuanza kupiga hatua za taratibu za kurudi kwangu mtaa wa pili kutoka ninapo ishi.Nikiwa njiani nikastuka nikiitwa na sauti ya mtoto wa kiume huku akinikimbilia akinifwata sehemu nilipo
"Shikamoo Sir Eddy"
"Marahaba hujambo mtoto mzuri?"
Nikaanza kujiuliza huyu mtoto amenijuaje wakati kwa makadirio ya macho yangu hajamaliza darasa la saba, kutokana na kimo chake pamoja na sura yake bado niyakitoto
"Sijambo"
"Unaitwa nani?"
"Jumaa"
"Jina langu amekuambia nani?"
Kikajichekesha kisha kikanijibu
"Ameniambia dada yangu yule pale nje"
Nikageuka kumtazama sehemu anayo nionyesha nikaona wadada wanne wakiwa wamekaa kibarazani wanacheza karata huku macho yakitutizama kwa kuiba iba, nikawasalimi wakaitikia kwa pamoja
"Haya rafiki yangu nenda kacheze"
"Sir Eddy naweza kuja kutazama DSTV kwako"
Nikajikuta nikiguna kimoyo moyo kwani sijui huyu mtoto amejuaje nimenunua DSTV wakati mimi minaishi mtaa wa mbele kutoka pale
"Mbona usiku labda kesho utakuja si unapajua kwangu?"
"Ndio ila leo kuna mechi za mpira ligi ya uingereza"
"Mmmm unashabikia timu gani?"
"Madrid ila uingereza nashabikia Liverpool"
Sikuwa na jinsi za kumkubalia akawaaga ndugu zake na tukaondoka.Tukafika kwangu nikamuwekea mechi ya mpira anayo itaka kupitia akaanza kuangalia huku akionekana kufurahi sana
Nikafungua kifuko changu cha chipsi nikamkaribisha Jumaa hakufanya makosa akaanza kuokota mskaki huku akiokota na chipsi nyingi
"Leo nitalala njaa"
Nikajisemea kimoyo moyo huku Jumaa akizidi kunichezea rafu kwenye kula hadi tukamaliza kwa hesabu za haraka haraka nimekula chispi kama ishirini tu kati ya nyingi zilizopo kwenye kifuko changu
Nikafungua friji na kumpa Jumaa soda akaonekana kuzidi kufurahi huku akipata midadi ya mpira unao chezwa
"Dogo saa nne huogopi kwenda kwenu?"
"Hapana si hapo nyuma tu"
Ikanibidi nikae kimya,dakika tano mbele mlango wangu ukagongwa huku sauti ya dada nisiye mjua akiita jina la Jumaa