SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 25 Novemba 2017

T media news

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU


Mtunzi: Bikora saidy
Sehemu ya pili( 02)

Endelea Nayo

Sarah chumbani kwake aliwaza  kwa muda sana akijiuliza  kama Wangesi anasimamisha jogoo lake hakuweza kupata jibu la  moja kwa moja maana wangesi alikuwa busy sana na maisha yake

Kitu ambacho marafiki wa kiume walianza kumchukua kulingana na kutoungana nao katika suala la kufuatilia wasichana miezi ilienda na mwaka ulikaribia kuisha

 Mtihani wa mwisho ulifanyika wa kuhitimu ufundi wangesi alikuwa mtu wa pili kwa ufaulu mzuri wenzake wote waliokuwa wakimcheka waliangukia pua hawakuweza kufauli mtihani ule

 Sarah nae hakufanikiwa kujua ukweli kwa wangesi kama yuko sawa

Baada ya mitihani kuisha wangesi alielekea nyumbani kwao huku akiwa na vyeti vizuri cheti cha udereva na utengenezaji magari alijisemea hapa malengo yangu yanaelekea kutimia sana maana njia hii nitahakikisha nafanya vitu vya maana .

Wangesi alivyofika nyumbani akiendelea na kazi zake na alipokuwa akilima ilikuwa ni karibia na barabara sema tu ni barabara ambayo ilikuwa haina lami yaani yatope tu!

Aliendekea kulima huku akiwa ameacha vyeti vyake vya udereva ndani japo akiwaza kuwa siku moja ataondoka kwenda mjini kutafuta kazi ya kufanya alianza kutafuta hela ya kutosha endapo akienda mjini asihangaike na maisha ya huko

 Wakati anaendelea kuandaa shamba muda huo ilikuja PRADO moja na muda huo mvua ilikuwa imenyesha dereva wa gari lile alishindwa kuendesha katika mazingira yale maana tope lilikuwa kubwa sana hivyo gari lilianza kurudi nyuma bahati nzuri gari lilisimama pembeni

Dereva alishuka chini huku akiangalia tatizo ni lipi na alijua tatizo ni barabara maana kulikuwa na tope sana!

Muda huo wangesi alimuangalia dereva wa Prado ile anavyohangaika na kutapatapa pale wangesi alitabasam na kujisemea sijui nikamsaidie yule lakini watu wa aina hii wanajiona sana hujihisi wanajua kila  kitu

Ngoja niache kwanza Wangesi aliendelea kumuangalia dereva yule mwisho alichukua upanga wake na kuelekea kwenye gari lile alipofika dereva hakuweza kumjari sana aliendelea kuwa busy na sim yake huku akitafuta msaada kutoka mjini

 Wangesi alimsalimia tena lakini dereva alimjibu kwa nyodo!

Habari kaka alisalimia wangesi
Fresh kwan vipi alijibu dereva
Hapana kaka nimeona unahangaika hapa muda mrefu Mimi nilikuwa naanda shamba pale hivyo nimekuja kujua tatizo ni nini  tusaidiane hat kwa mawazo
Hata kama ukijua huwez kuwa na msaada wowote hapa kama nimeshindwa Mimi mtoto wa mjini utaweza wewe mtoto wa shamba we endelea kuandaa shamba
Hapana kaka mawazo tu ni msaada tosha alisema wangesi
Hebu toka kwanza huend wew unataka kuniibia alisema dereva

Gafl sauti ya msichana ilitoka ndani ya gari lile ikilalamika majibu ya dereva wake alianza kumtetea Wangesi alisema ahaaaaaaaaaa kaka muache atusaidie bwana mbona hivo huyu ni mwenyeji wa sehemu hii huenda akawa anapafahamu vizuri embu mpe nafasi atusaidie!

Dereva alisema na wew Monica endelea kukaa huko huku hayakuhusu Mimi niko na huyu jamaa

Monica alisema kaka tunachelewa embu mruhusu atusaidia maana muda unaenda sana!

Hapo dereva alimuita wangesi aliyekuwa ameshaanza kuzipiga hatua kadhaa kuelekea shambani kwake ailiita we jombaaaaaa brother nakuomba kidogo .

Wangesi aligeuka na kusimama muda huo alirudi kwa ajili ya kumsikiliza dereva yule wangesi alifika na kuitika wito

Dereva alianza kuomba radhi na kusema samahani kaka naomba utusaidie nisamehe kaka!

Wangesi hakuweza kuongea kitu alijisemea ufundi wangu utakujibu pumbavu wew.

Muda huo wangesi alifunua gari mbele ya bodi na alianza kutengengeneza na alikuta hitirafu kwenye betry ya gari kuna waya ulikatika hivyo aliunga kufunika tena derveva wa gari lile hakuwa na ujuzi wowote zaidi ya kuendesha tu!

Wangesi alimaliza na aliingia ndani ili kuendesha gari lile duuuuu alipoingia alikutana na msichana nzuri sana kiasi kwamba alihisi mwili kusisimuka alijikaza na kuanza kulitoa gari mahali pale na kulipeleka sehemu nzuri

Alifanikiwa kuliwasha na kulitoa sehemu ile muda huo Monica aliyekuwa amekaa nyuma alianza kuvutiwa na kazi nzuri ya kijana Wangesi baada ya Wangesi kuhakikisha kuwa gari liko sehemu salama alimgeukia Monica alitabasam na kusema mnaweza kuendelea na safari gari iko salama

Monica alishukuru na dereva wake aliingia na kuanza kuendesha gari lile!
Monica alianza kufikilia tabasam la kijana Wangesi

Wangesi alizipiga hatua kuelekea shambani kwake!

      Usikose sehemu ya tatu( 03)