Katika hali isiyo ya kawaida, watu wanaodhanikiwa kuwa wezi wa mitandao wametumia simu ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo kujipatia TZS 4 milioni.
Mkuu wa Wilaya alisema kuwa mapema Alhamisi, Februari 22 mwaka huu alitumiwa ujumbe katika simu yake ukieleza kwamba namba yake imezuiwa (blocked), na hivyo anatakiwa kusajili upya, kwa sababu hakuwa akiweza kupika au kutuma na kupokea jumbe (sms).
Chonjo aliyasema hayo akizungumza na waandishi wa habari na kusema watu hao waliodukua simu yake, walitumia namba yake kujipatia fedha kutoka kwa watu mbalimbali.
DC Chonjo amesema ameripoti tukio hilo polisi ambapo alipata taarifa kutoka kwa rafiki zake wawili ambao walisema kwamba walipokea jumbe zikiwataka kutuma fedha kwenye namba hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Mtei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, hadi sasa watu watatu wamekamtwa wakihusishwa na tukio hilo.
Aidha, ameongeza kuwa uchunguzi wao umebaini kuna kundi la watu ambalo hudukua namba za simu za mkononi za watu mbalimbali na kutumia kujipatia fedha.