Huduma ya kwanza ni huduma ya haraka na ya muda anayopewa mwathirika wa ajali au ugonjwa wa ghafla. Madhumuni yake ni kulinda maisha, kusaidia kufufua na kuzuia madhara ya hali hiyo, mpaka huduma ya daktari itakapopatikana kwa kwenda hospitali au nyumbani kwa majeruhi. Umuhimu wa huduma ya kwanza unajidhihirisha kutokana na masanduku ya huduma ya kwanza kuonekana katika mabasi, treni, kumbi zasinema , migahawa na hoteli, katika shule na vyuo na karibu katika maeneo yote ya umma na nyumba za watu wote wanaojali afya.
Vitu hivi vinahitajika katika sanduku la huduma ya kwanza:
1.Plaster au bandage zinazonata salama kwa ajili ya kufunga vidonda vidogo
2.Gauze safi na salama kwa ajili ya kufunga majeraha makubwa
3.Maji safi na salama
4. Crepe bandage
5.Mkasi
6.Dawa ya maumivu mfano panado au aspirin
7. Bandage za pembe tatu
8. Mipira ya mkononi(gloves)
9.tweezer kwa ajili ya kuondolea vipande vya vitu kwenye ngozi
10.Daftari au notebook kwa ajili ya kuandika mambo uliyofanya
11. Spirit antiseptic
12.Pamba (cotton wool)
13. Sindano au pini
13. Sindano au pini