SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 8 Agosti 2016

T media news

Mwanamichezo wa mara ya kwanza Mmarekani ashiriki Olimpik akiwa kavaa hijab

Ibtihaj Muhammad anasema anapenda michezo, lakini mara kwa mara anataabika kutafuta mahala panapomfaa katika michezo.

Siku ya tatu ya michezo ya Olympik huko Rio itaangalia matukio ya medali katika michezo ya sarakasi, kuogelea, kuruka viunzi, rugby kwa wanawake na michezo mingineyo. Washiriki wa mara ya kwanza katika michuano hiyo pia wanashindana katika siku ya tatu.

Ibtihaj Muhammad, mwanamichezo wa mara ya kwanza raia wa Marekani akishiriki michuano hiyo akiwa kavaa hijab yake atakuwa miongoni mwa wanaoshindania medali leo. Ni muislam aliyekulia katika jimbo la New Jersey, Ibtihaj mwenye umri wa miaka 28 anasema anapenda michezo, lakini mara kwa mara anataabika kutafuta mahala panapomfaa katika michezo.

Alianza kuruka viunzi mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka 13. Alionyesha kipaji chake kwenye timu ya taifa ya Marekani mwaka 2007 wakati alipogundua kwamba hakukuwa na kundi la walio wachache wanaowakilishwa. Mwaka 2011, Muhammad alikuwa mwanamke wa kwanza mwanamichezo muislam kuiwakilisha Marekani. Alikuwa wa pili Marekani na namba 12 duniani kote