Huduma za mitandao ya kijamii zimefungwa nchini Ethiopia.
Mapambano ya wikiendi kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama nchini Ethiopia yanadaiwa kusababisha vifo vya zaidi ya watu darzeni moja kote nchini humo huku mamia wakikusanyika katika maandamano ya kuipinga serikali katika mji mkuu baada ya wito kutolewa kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP serikali ya Ethiopia kwa mara nyingine imezuia huduma za mtandao wa internet mwishoni mwa wiki ikishutumu kuwepo ‘watu wanaovuruga amani, waliopo nje ya nchi na kuungwa mkono na wanaharakati wa kwenye mitaandao ndio wa kulaumiwa kwa ghasia hizo.
Waandamanaji walikusanyika licha ya onyo la serikali kwamba itachukua hatua dhidi ya maandamano yasiyoruhisiwa.
Chanzo VOA