Rais wa Marekani, Donald Trump amemjia juu Mwandishi aliyemuuliza kama ni kweli Urusi inaisaidia kuipa Iran taarifa za kiintelejensia ili kuipa urahisi Iran kuzishambulia silaha za kivita na Wanajeshi wa Marekani.
Trump amejibu "Hilo ni tatizo kuliko tatizo tulilo nalo, nakuheshimu sana Mwandishi ila hilo ni swali la kijinga kuulizwa muda huu, tunaongelea mambo mengine hapa"
Itakumbukwa Washington Post jana iliripoti kuwa Maafisa wa Marekani wamedai Urusi inasaidia kuipa taarifa Iran ya zilizopo meli na ndege za kivita za Marekani pamoja na vifaa vingine vya kivita ili iwe rahisi kwa Iran kuishambulia Marekani.
