Habari sanaa na michezo

Ijumaa, 6 Machi 2026

T media news

HIVI UMESHAWAI KUJIULIZA KWANINI RAIS WA ISRAEL HASIKIKI ANASIKIKIA WAZIRI MKUU TU?

 

Kupitia vita hii najua wengi mmekuwa mnajiuliza mbona Israel anasikika tu Waziri Mkuu akifanya mahojiano na maamuzi pia? Kwani Israel haina Raisi?


Ukweli ni kwamba Israel ina raisi ila mfumo wao wa kiutendaji na jinsi wanavyo patikana ni tofauti kabisa na jinsi Raisi wetu wa Tanzania na waziri wake wanavyo patikana.


Hapa chini nimekueleza hatua Kwa hatua Ili upate ukweli ni kwanini Waziri Mkuu wa Israel Benjamin netanyahu ana nguvu kuliko raisi.


Mfumo wa uongozi wa Israel bwana uko hivi.


1, Rais anapatikanaje?


Rais hachaguliwi na wananchi moja kwa moja,

Wabunge wa bunge la Israel (Knesset) ndio wanaompigia kura.


Bunge hilo lina wabunge 120, na wao humchagua rais kwa kura.

Rais anahudumu kwa kipindi cha miaka 7.


Kazi ya rais ni zaidi ya heshima na kuwakilisha taifa, sio kuongoza serikali kila siku.


2, Waziri Mkuu anapatikanaje?

Wananchi wa Israel hupiga kura kuchagua wabunge wa bunge lao linaloitwa Knesset.


Baada ya uchaguzi, chama au muungano wa vyama wenye wabunge wengi huunda serikali.

Kiongozi wa chama hicho huwa Waziri Mkuu.

ambaye ni Benjamin Netanyahu sasa,


Yeye ndiye mwenye nguvu kubwa serikalini:

Anaongoza serikali

Anaongoza maamuzi ya kisiasa na kijeshi

Anaongoza baraza la mawaziri.


Kwa kifupi ndani ya Israel hao viongozi hupatikana hivi.


Wananchi wanachagua wabunge.

Wabunge  wanachagua Rais.

Chama chenye wabunge wengi kiongozi wake anakuwa Waziri Mkuu


3, Kwanini wanafanya hivi?


Ili kuzuia mtu mmoja kuwa na nguvu nyingi

Katika mfumo huu, nguvu zinagawanyika.


Rais anakuwa wa heshima na kuwakilisha taifa.

Waziri Mkuu anaongoza serikali lakini bado anategemea bunge.


Hii husaidia kuzuia kiongozi mmoja kuwa na mamlaka makubwa sana kama ilivyo kwa Rais wa United States (Marekani).


Vipi umejifunza Nini?