SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 15 Novemba 2017

T media news

Polisi Nchini Zimbabwe 'Wadhibitiwa' na Jeshi Harare

Mwanasheria mmoja katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare amepakia kwenye Twitter picha inayoonyesha kundi la maafisa wa polisi wakiwa wameketi kwenye foleni, huku wakiwa chini ya uangalizi wa maafisa wa jeshi.

Fadzayi Mahere, ambaye anapania kuwa mbunge wa Mount Pleasant, Harare, anasema alipiga picha hiyo kupitia dirisha la afisi yake.

Haijabainika nini kilikuwa ninatokea kwenye picha hiyo.