Katika maeneo mengi ya Afrika mashariki hususani Tanzania tuna kiasi kikubwa sana cha maji kwenye mito, chemichemi, maziwa na maji ya ardhini(undergroundwater) ambapo asilimia 70% hutumika kwenye kilimo kwa kuzalisha mazao mbalimbali
Lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi mvua iliyokuwa ikitegemewa sana na wakulima kama chanzo cha maji kwa mimea imekuwa sio ya kuaminika tena kwani hainyeshi tena kwa wakati, hunyesha kwa kiasi kidogo sana(450mm-600mm), maeneo mengine hunyesha kwa kiasi kikubwa sana mpaka kusababisha mafuriko ambayo huharibu vibaya mazao ya wakulima mashambani, pia baadhi ya vyanzo vya maji vimekauka na hivyo kusababisha uhaba mkubwa sana wa maji sio tuu kwenye kilimo bali hata kwenye upatinaji wa maji safi kwa matumizi ya nyumbani
KWA NINI TUVUNE MAJI YA MVUA
Kama nilipoeleza hapo awali kuwa kuna baadhi ya maeneo mvua hunyesha kwa kiasi kidogo sana na hivyo hazitoshelezi kumalizia msimu mzima ili mazao yaliyo shambani yaweze kukomaa mfano wa maeneo hayo ni Rombo, Same, Lushoto,Baganoyo,kisarawe,mkuranga n.k pia maeneo ya mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora n.k ambapo mvua inayonyesha katika maeneo haya inakadiriwa kuwa 550mm kwa mwaka, hali hii imesababisha matatizo makubwa sana katika maeneo hayo kama kukosekana kwa maji safi, baa la njaa, kipato kidogo kwa wakulima kwani hutegemea sana kilimo
Kwa kuliona hilo makala hii itakusaidia kujua namna ya kuvuna maji ya mvua ili yatumike katika umwagiliaji pale mvua zinapokatika ili kuongeza mavuno kwa wakulima na waweze kuondokana na umaskini pia utegemezi kwa serikali kwa kutoa chakula cha msaada
MAMBO YA MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA KUTENGENEZA LAMBO
I.Sura ya eneo husika(topography and terrain)
Hili ni la muhimu sana katika kuangalia sehemu ya kutengeneza lambo la kuhifadhi maji ya mvua, itabidi kuangalia kwa kitaalamu eneo ambalo maji yanatoka ili yaje kwenye lambo lenyewe(catchment area) pia lazma ifanyike survey ya eneo ambalo lambo litajegwa ili kuzuia mchanga au udongo kujaza lambo lako inabidi utaalamu wa kihandisi utumike.
II.Kiasi cha mvua kinachonyesha katika eneo husika
Hii itakusaidia kujua na kukadiria kiasi cha maji unachoweza kuvuna pia ukubwa wa lambo kwa ajili ya kutosheleza mahitaji yako
III. Aina ya udongo
Udongo ni muhimu zaidi katika kuchagua na kuweza kujua kiasi cha maji kitakacho hifadhiwa katika lambo lako, pia data za udongo zitamsaidia mtaalamu kukuambia ni zao gani unatakiwa ulime pia ni kiasi gani cha maji kinachotakiwa wakati wa kumwagilia ili kupunguza upotevu wa maji na kusaidia mimea kukua vizuri
NAMNA YA KUTENGENEZA LAMBO
Awali ya yote kabla ya kuanza kutengeneza lambo lenyewe ni kuandaa njia ya kuyakusanya maji(runoff concentration) kutoka kwenye sehemu mbalimbali kama kwenye mifereji ya barabara, maeneo ya wazi kama maeneo ya kuegesha magari, maji yanayotoka kwenye makazi ya watu(rooftop water concentration) kwa hapa unaweza kutumia mawe (stonebudds) matuta ili kuzuia maji na kuyaelekeza kwenye mrefeji unaoingia kwenye lambo ila matuta hayo lazima yapimwe kitaalamu ili yasiharibiwe na maji endapo mvua itakuwu nyingi
Kinachofuata baada ya hapo ni namna ya kutengeza mfereji unaopeleka maji maji kwenye lambo(grit channel design and filter drain), kwa kuwa maji yanayokuja huwa na michanga, udongo au tope ambayo yakiingia kwenye lambo lako husababisha lambo kujaa mapema na kuhifadhi kiasi kidogo cha maji, kwa hyo sasa mfereji huu inatakiwa uwe na usanifu mkubwa hasa kwenye mteremko wake(slope) ili kuzuia mchanga,matope na udongo kuingia kwenye lambo lako
Baada ya hapo lambo linatakiwa lichimbwe kwa ustadi kwa kufuata vipimo husika ili kuweza kuhifadhi kiasi cha maji kinachotakiwa pia kulingana na aina ya udongo katika eneo lako kitaalamu tutakuambia ni aina gani ya material yanayohitajika kwa ajili ya kuweka kwenye lambo lako ili maji yasipotee mfano unaweza kuweka karatasi ngumu za nylon (polythene papers) pia maeneo mengine yanahitaji tuu kushindilia vizuri ardhi ya chini ili iwe imara na isiruhusu maji kuzana chini.
FAIDA ZA KUVUNA MAJI YA MVUA
a)Kuvuna maji ya mvua inahitaji gharama ndogo sana lakini maji yanayovunwa ni mengi na huweza kutosheleza mahitaji ya mimea yako hata kama una shamba la hekari kumi endapo utaalamu utamika vizurib)Maji yanayovunwa humpa mkulima uhuru wa kuyatumia atakavyo pasipo kubugudhiwa kwa sababu hayana bili wala malipo unapotumiac)Maji huvunwa na kutumika mahali husika kwa hiyo hakuna gharama sana za kuhitaji mabomba ya kusafirishia maji hayo
Pia kwa ujumla uvunaji wa maji ya mvua ndio suluhisho pekee la kutatua matatizo ya maji katika maeneo ammbayo yana uhaba wa maji na yanayokubwa na ukame kwa kipindi kirefu
Pia kuna utaalamu mwingine wa uvunaji wa maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kwa ajili ya mifugo
Katika jamii zetu kama utaalamu huu utakuwa endelevu tutasaidika kwa kupata chakula cha kutosha, kuongoze kipatao na pia kuboresha maisha ya watanzania wengi kwa ujumla.