SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 24 Novemba 2017

T media news

Onyo la serikali kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inawataarifu wananchi kuhusu orodha ya viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kama ilivyo sasa. Lengo ni kuwawezesha wananchi kuwafahamu viongozi wa vyama vya siasa, kwani imedhihirika kuwa wananchi wengi hawawajui viongozi wengi wa vyama vya siasa na nafasi zao.

Napenda watanzania wafahamu kuwa, orodha ya viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa hubadilika pale ambapo muda wa uongozi wa viongozi wa kitaifa umeisha na viongozi wengine kuchaguliwajkuteuliwa, kiongozi kujiuzuru, kufariki au kuondolewa katika uongozi au uanachama.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ndiyo yenye dhamana ya kuhifadhi taarifa za viongozi wa kitaifa wa kila chama siasa. Hivyo, imekuwa na utaratibu wa kuujulisha umma mara kwa mara na kwa njia mbali mbali, kuhusu orodha ya viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa mara panapotokea mabadiliko ya uongozi.

Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 8A na 8B cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 [RE: 2015] kama ilivyorekebishwa mwaka 2009, ni kosa la jinai kwa mtu yeyote ambaye hatambuliki na Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa ni kiongozi wa kitaifa wa chama cha siasa, kufanya shughuli za chama au siasa kwa niaba ya chama chochote cha siasa.

Msajili wa Vyama vya Saisa anawaasa wanachama wa vyama vya siasa kuheshimu Sheria za nchi, hasa Sheria ya Vyama vya Siasa.

Sisty L.  yahoza

Kny: MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

23 Novemba, 2017