SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 16 Novemba 2017

T media news

Dkt. Shika ni Baraka Toka kwa Mungu- Kala Jeremiaha

Msanii Kala Jerimah amewataka watu kumpenda na kumthamini Dkt. Louis Shika, kwani mzee huyo ni mpango na baraka kutoka kwa Mungu kwetu sisi Watanzania.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Kala Jeremiaha ameandika ujumbe akisema kwamba amemsikiliza kwa makini mzee huyo ambaye hivi sasa ni maarufu hapa bongo, na kusema kwamba haijalishi madhaifu aliyonayo, ila ana hakika ni mpango wa Mungu na baraka zake kuwepo kwake duniani.
“Nimesikiliza kwa makini sana maelezo ya mzee wetu. sitaki kuongelea utajiri wake wala umaskini wake nataka kuongelea majaribu aliyokutana nayo katika safari ya maisha yake. Ni wazi kuwa mzee huyu yupo duniani kwa kuwa mungu kamchagua na Mungu humchagua mtu kwa kusudi lake. Nionavyo mimi mzee huyu ni baraka kutoka kwa Mungu haijalishi madhaifu yake ila kwa uhakika ni mpango wa mungu kuwepo kwake kwetu”, ameandika Kala Jeremiah.
Kala ameendelea kuandika akisema kwamba ...”niwaombe wanajamii tumuonee huruma na tumpende, hicho ndicho kitu pekee anachohitaji mzee huyu na kwa hakika amekikosa kwa miaka mingi, haitakugharimu chochote kumhurumia na kumpenda, nawaomba”.
Dkt. Louis Shika alipata umaarufu wiki iliyopita baada ya kutangaza kununua nyumba zinazopigwa mnada na serikali za bilionea Lugumi, na kutaja kiasi kikubwa cha pesa huku mfukoni hana pesa yoyote, kitendo kilichosababishwa apelekwe polisi na kuwekwa rumande.