SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 16 Novemba 2017

T media news

Msigwa Hatupa Dongo Hili kwa Wanaohama Chama "Siasa za Upinzani wa Tanzania ni kwa Wanaume na Sio kwa Wavulana"

Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa ametupa maneno yanayodaiwa kuwa ni 'kijembe' kwa wale wanaohama chama cha upinzani na kuwaambia kwamba upinzani ni kwa wanaume na si wavulana.

Msigwa ameweka 'kijembe' hicho kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwa ni siku moja tangu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mstaafu, Lawrence Masha kutangaza kujiondoa ndani ya chama hicho.
"Siasa za upinzani wa Tanzania ni kwa wanaume na sio kwa wavulana,  wavulana wana visingizio vingi kwa nini haliwezekani, sisi wanaume tuna sababu moja kwa nini inawezekana. Unajua nini? Tunatenda lililo sahihi," Msigwa
Viongozi mbalimbali kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo wameweka wazi kwamba kuondoka kwa Masha kwenye chama chao ni haki yake ya kidemokrasia lakini pia wamemtaka atoe sababu za kweli za kuondoka na siyo zile alizoziandika kwenye barua ya kujivua.