SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 16 Novemba 2017

T media news

Ndugai Awaamshia Dude Mawaziri "Waheshimiwa Acheni Kupiga Story Bungeni Wasikilizeni Wabunge"

Spika wa Bunge, Job Ndugai amewataka mawaziri waache kupiga stori bungeni na kusikiliza wabunge wanapouliza maswali.

Ndugai ametoa agizo hilo leo Alhamisi asubuhi wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni.

“Kipindi cha maswali waheshimiwa mawaziri acheni kupiga stori… waheshimiwa mawaziri hamsikilizi,’’ amesema Ndugai

Kauli ya Ndugai imekuja baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Mwantumu Dau Haji kuuliza swali la nyongeza kuhusu kilimo cha umwagiliaji alilolielekeza kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira.

Wakati akiruhusu naibu waziri kujibu swali hilo, Spika amesema kuwa swali hilo lilipaswa kujibiwa na wizara ya maji hivyo kumtaka naibu waziri wa wizara hiyo kujibu.

“Hilo swali lilitakiwa liende Wizara ya Maji, Naibu Waziri Maji, Mh Aweso (Jumaa),” Ndugai alimtaka Naibu Waziri wa Maji kujibu swali na kuongeza kuwa, “ndo shida mnakuwa mnaongea, hamsikilizi humu ndani, jibu swali.”

Baada ya hapo, Spika alimwambia Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano, Kangi Lugola kujibu swali hilo. “Mh Kangi Lugola okoa jahazi’ alisema Ndugai ambaye alikuwa akiwasisitiza mawaziri kuwa makini kusikiliza.

Pia, Spika amewataka baadhi ya mawariri kujiandaa kutoa majibu mafupi katika maswali yanayohusu wizara zao, “Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Afya, Wizara ya Maji kwa majibu yanayokuja na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa majibu yanayokuja, ni marefu sana mawaziri wawe wanatoa majibu kwa ufupi,” amesema