SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 13 Agosti 2017

T media news

Chelsea kufungwa na Burnley ni habari mbaya, lakini hii hapa ni habari yao mbaya zaidi

Hapo jana Chelsea walikuwa uwanjani wakikabiliana na Burnley ambapo Burnley waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao matatu kwa mbili katika uwanja wa Stamford Bridge.

Kipigo hiki kimeanza kuleta hofu kwa mashabiki wa Chelsea huku wengi wakianza kusema ule utabiri wa wao kuboronga msimu huu umeanza kuonekana mapema.

Kinachowanyima sana raha Chelsea ni kuhusu mechi ijayo ambapo itawalazimu kuwafuata Tottenham Hotspur katika mchezo ambao unaweza kuwa mgumu zaidi.

Habari mbaya zaidi ni kwamba katika mchezo kati ya Chelsea na Tottenham Hotspur wachezaji 6 muhimu katika kikosi hicho watakuwa nje ya uwanja kwa sababu tofauti tofauti.

Eden Hazard bado anaendelea kutibu majeraha yake aliyoyapata akiwa na timu ya taifa huku Tiomoue Bakayoko akiwa nje akiendelea kutafuta fitness.

Garry Cahill atakuwa akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata jana dhidi ya Burnel kama ilivyo kwa Eden Hazard huku Pedro Rodriguez akitumikia kadi nyekundu aliyopata katika mechi ya ngao ya hisani.

Diego Costa naye bado hajarudi klabuni hapo akiendelea kufuatilia masuala yake ya uhamisho ambapo inadaiwa yuko njiani kurejea katika klabu yake Atletico Madrid.

Hii inawafanya Chelsea kwenda kukabiliana na Tottenham huku 60% ya wachezaji ambao walikuwa wakianza nao msimu uliopita wakiwa nje ya uwanja katika mchezo huo.