Miss Tanzania mwaka 2001, Happiness Millen Magese ambaye anafanya kazi ya uwanamitindo amebahatika kupata mtoto wake wa kwanza Julai 13 mwaka huu.
Millen amewahi kumwaga machozi hadharani akielezea mateso yanayotokana na tatizo aliloligundua kwake toka akiwa na umri wa miaka 13 la mirija yake kuziba mwaka 2007.
Kuna kipindi alikata tamaa mpaka akajiandaa kuondoa kizazi na hapo ni baada ya kufanyiwa oparesheni zisizopungua 13 ambapo pamoja na hayo, aliambiwa moja ya tiba ya tatizo hilo liitwalo ‘Endometriosis’ kwa kizungu, ni kuzaa.
Baada ya mateso yote usiku na mchana pamoja na kutumia gharama kubwa kwenye matibabu South Africa na Marekani, hatimaye amefanikiwa kupata mtoto wa kiume July 13 2017 Hospitalini New York Marekani na anaitwa Prince Kairo Michael Magese.