Mkongwe wa muziki nchini Tanzania TID alikuwepo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM akiwa anarelease ngoma yake mpya ambayo inaitwa “Maisha ya Jela” aliyomshirikisha rapper Fid Q.
Tittle ya ngoma hiyo mpya ya TID inaendana kabisa na matatizo ambayo amepitia siku hizi za karibuni mkali huyo kutokana na sakata la madawa ya kulevya lililo tikisa jiji la Dar es Salaam siku chache zilizopita.
Ni mengi ambayo aliyazungumza TID kwenye interview hiyo ila kubwa zaidi ni huu mtazamo wake kuhusu vijana wengi kushindwa kujinasua kwenye dimbwi la madawa la kulevya.
“Kwa experience yangu mimi nahisi ni kwasababu hawataki kuyabadilisha maisha ambayo walikuwa wanaishi hapo awali. The best way to win this thing ni kubadilisha system yako ya maisha, badilisha marafiki itakusaidia.” Alisema TID.