SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 21 Februari 2017

T media news

Mzee wa Miaka 98 Aoa Bibi wa Miaka 88 Baada ya Kuishi Wote Miaka 60 Wakichunguzana..!!!


Kweli nimeamini mapenzi hayana mwenyewe na huku waswahili husema ukistaajabu ya Mussa…… hapo waweza malizia mwenyewe. Hii tunaiona kwa Mzee Willy Kinyua (98) baada kufunga ndoa na Joyce Nyambura (88) baada ya wenza hao kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka 60.

Hehehe, Wengine wetu wasipoona ndoa mapema hulalamika na kukata tamaa, Je ungekuwa Joyce ingekuwaje baada ya kuishi na bwana huyo miaka hiyo 60, hatuwezi kusema sana ila lahasha! yawezekana mzee Willy aliupanga huo muda ndio wakati sahihi wa kumuona Mwanamke huyo.

Wanandoa hao wamefunga ndoa katika Kanisa la Ubatizo lililopo Solai kwenye Kaunti ya Nakuru nchini Kenya huku wakiwa na watoto 5, huku sasa wakitembea kwa fimbo.

Aidha Kinyua alisema kuwa alikuwa miongoni mwa waliopigana vita ya MauMau na kwamba, ingawa alikuwa porini kwa miaka tisa, Nyambura hakumsaliti. “Nampenda Nyambura, ni mwanamke mrembo ambaye kila mara amekuwa chanzo cha nguvu zangu na kunitia moyo. Hajawahi kunisaliti.”

Kwa upande wake Nyambura amesema, amefurahi kusheherekea ndoa yake kama ambavyo kila mwanamke angependa iwe hivyo, huku akidai kuwa alimpenda sana Kinyua na kwamba walikuwa wakiishi kwa imani.