Ni nadra sana kukuta msanii wa Afrika anafikiriwa kuwa kipaumbele kwa lebo yoyote kubwa ya kimataifa hasa kama Sony Music, lakini kwa nyuzi kali za Bad Man Wizzy ni wazi kuwa wasanii kutoka Afrika wamekuwa wagumu kuwapotezea.
Mkali wa muziki nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahim ‘Wizkid’, adaiwa kuwa ndani ya mwaka huu project zake nyingi zitapewa backup kubwa sana na lebo ya kimataifa Sony Music, na kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa, Sony Music imetangaza kuwa kwa mwaka huu Starboy Wizzy ni kipaumbele chao cha kwanza kuhakikisha kuwa staa huyo anafikia malengo yake ya kuwa a Super International star.Sony Music kupitia wakurugenzi wake wa RCA Records wamethibitisha tetesi zinazosambaa juu ya maamuzi hayo kupitia press statement inayosema.. “New RCA priorities in 2017 include 18-year-old Texan Khalid, All My Friends singer Tinashe, Nigerian One Dance collaborator Wizkid, hip-hop artist Goldlink and band Muna.”Hii hapa tafsiri ya ujumbe huo.. “Vipaumble vipya wa RCA Record kwa mwaka huu wa 2017 ni pamoja na Texan Khalid mwenye umri wa miaka 18, Tinashe mwimbaji wa single ya ‘All My Friends’, Msanii aliyeshirkishwa kwenye wimbo wa ‘One Dance’ Wizkid, Hip Hop artist Goldlink na Band Muna”Miezi kadhaa iliyopita Wizkid aliweka wazi kupitia kurasa zake za social media kuwa huenda mashabiki wake wakapokea ‘album 4 kutoka kwake mwaka huu wa 2017′, na kwa muonekano wa mambo ni wazi kuwa mwaka wa 2017 umeanza poa sana kwa Mnigeria huyo.
Source: MTV Base