SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 21 Februari 2017

T media news

ADAMA BARROW ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA

Rais wa Gambia, Adama Barrow ambaye ameapishwa rasmi siku ya jumamosi ya Februari, 18 wakati taifa hilo likiadhimisha miaka 52 tangu kupata uhuru ameanza kutumikia nchi hiyo kama Rais kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 174.

Taarifa ya kusamehewa kwa wafungwa hao, ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo, Mai Fatty wakati alipofanya ziara katika moja ya magereza na kuelezea kuwa licha ya msamaha huo lakini pia serikali inayoongozwa na Barrow imejipanga kuboresha mazingira ya wafungwa.

“Tutaboesha mazingira ya ambayo wanakuwepo wafungwa ili tuwe katika viwango vya kimataifa, maboresho katika magereza yetu ni muhimu,” alisema Waziri wa Mambo ya Ndani wa Gambia, Mai Fatty na kuongeza.

“Tumekusudia kuwabadilisha wananchi wetu wenye tabia mbaya kuwa na tabia nzuri, wasio na ujuzi wapate ujuzi na ambao hawana elimu wapate elimu.”