SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 7 Februari 2017

T media news

Kamanda Sirro :Tumemkuta Wema na Misokoto ya Bangi na Makaratasi Yake,Hivyo Naye Atapanda Mahakamani Tu ..!!!!



Sakata la wasanii 12 wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi limezidi kukua baada ya watu wengine 100 kukamatwa.

Kati ya watu 112 ambao wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kujihusisha na utumiaji au biashara ya dawa hizo, 12 kati yao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo baada ya kazi hiyo kushindikana jana.

Miongoni mwa watuhumiwa wanaotarajiwa kupandishwa kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ni mwigizaji maarufu wa filamu Wema Sepetu na msanii mwenzake Omary Micheri ambao polisi wamedai walikutwa na vielelezo vya dawa za kulevya na bangi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Siro alisema watawafungulia watuhumiwa maombi ya kuwaweka chini ya uangalizi wa mahakama na polisi kwa muda wa miaka miwili na watakuwa wakiripoti kituo cha polisi mara mbili kwa mwezi.

Siro alisema kati ya watuhumiwa 12 waliokamatwa kwanza, 10 walikiri kutumia dawa hizo na kuwataja wauzaji lakini wawili walikutwa na vielelezo nyumbani kwao.

Alisema Wema, ambaye aliwahi kushinda taji la mrembo wa Tanzania (Miss Tanzania), alipekuliwa nyumbani kwake na kukutwa na misokoto ya bangi na makaratasi yake, wakati Micheri alikutwa na kete tatu za dawa za kulevya ambazo hazijajulikana za aina gani hadi zitakapofanyiwa uchunguzi.