SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 7 Februari 2017

T media news

JE Urafiki wa Kanye West na Trump Umevunjika ?

Kwa wewe mfatiliaji wa habari za burudani za nje pamoja na siasa za Marekani utakua unakumbuka issue ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rapa Kanye West kuwa na urafiki mkubwa kabla na hata baada ya kutangazwa kuwa Rais wa taifa hilo kubwa duniani.

Mtandao wa TMZ wa Marekani umeripoti kuwa inawezekana Kanye West na Trump urafiki wao umevunjika kwa kinachoaminika kuwa Kanye West kuchukizwa na vitendo vinavyoendela kwa Trump kwa kukataza baadhi ya mataifa ya kiislamu kuingia nchini humo.

Kabla ya Trump kuapishwa, Kanye West aliingia kwenye headlines za duniani kwa kutangaza wazi kumsapoti Trumpkwa kwenda mpaka Trump Tower na kukutana na Rais huyo wa Marekani,haya yote yanakuja baada ya Kanye West kufuta tweets zote alizokuwa akimsifia na kuonyesha imani na mapenzi yake kwa Rais huyo waMarekani.