SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 5 Oktoba 2016

T media news

Marafiki watano wa karibu wa Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo ni moja kati ya wachezaji bora duniani ambao dunia imewahi kuwashuhudia na watu wengi wangependa kuwa na urafiki na nyota huyu ambaye aliwahi kusema, ” Ninachojali ni familia, soka na pesa”.

Mtandao wa sokkaa.com umetoa orodha ya marafiki wakubwa watano wa Cristiano Ronaldo ambao ni…

5. Wayne Rooney – Manchester United

Nahodha wa England Wayne Rooney ni miongoni wa marafiki wakubwa wa Cristiano Ronaldo ambaye alijiunga na Manchester United mwaka 2004 mwaka mmoja baada ya star wa Ureno kujiunga na mashetani wekundu.

Wote kwa pamoja walisherekea mafanikio wakiwa chini ya Sir Alex Ferguson kwa kutwaa mataji ya Premier League na Champions League kabla Ronaldo hajahamia Real Madrid mwaka 2009.

4. Ricardo Quaresma – Beskitas

Winger wa Besiktas Ricardo Quaresma amekuwa akiitumikia timu ya taifa ya Ureno tangu mwaka 2003 sawa na Cristiano Ronaldo, wachezaji hawa wanafahamika kuwa ni marafiki wa karibu.

Waliisaidia timu yao ya taifa kushinda taji lao kubwa kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Euro 2016 kwa kuichapa Ufaransa 1-0.

3. Marcelo – Real Madrid

Ronaldo na Marcelo wametengeneza urafiki tangu Ronaldo alipotua Real Madrid akitokea Manchester United mwaka 2009.

Wamekuwa wakifurahia kutaniana wakati wa mazoezi na wakati wa kushangilia uwanjani kwenye mechi inaonesha namna gani walivyoshibana.

2. Pepe -Real Madrid

Pepe na Ronaldo ni marafiki wa karibu ambao wamekuwa wakicheza pamoja Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno tangu mwaka 2009.

1. Cristiano Ronaldo, Jr.( His Son)

Cristiano Ronaldo anamarafiki wengi ambao anatumianao muda mwingi pamoja lakini inapokuja suala la mtoto wake wa pekee, mambo yanabadilika – inadaiwa Ronaldo alistukia mpango wa mama wa mtoto wake kutaka kutoa mimba kabla hajazaliwa, Ronaldo anampenda sana kijana wake na muda mwingi akiwa nje ya uwanja amekuwa nae karibu.

Ronaldo amekuwa akikosolewa kwa kitendo chake cha kutomtaja mama wa mtoto huyo lakini ameonesha kwamba anaweza kumlea mtoto huyo bila uwepo wa mama yake.