Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi wanne waliokuwa wamejichimbia katika pori la Mbande jijini Dar es Salaam mara baada ya mapigano makali na majibizano ya risasi yaliyojiri kwa zaidi ya dakika arobaini.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Siro, amesema kuwa jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mmoja wa Majambazi aliyehusika na tukio la ujambazi CRDB Mbagala
"Polisi mara baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na tukio hilo akiwa na wenzie saba hivyo aliwaambia askari kuwa anawapeleka sehemu walipo wenzake kwenye pori la Dondwe ambapo wanafanya mazoezi ya kivita.
"Walipofika katika eneo hilo la mipakani Chanika gafla majambazi hayo yalianza kufyatua risasi kwenye uelekeo wa askari na mtuhumiwa alikimbia na askari wakaanza kujibu mashambulizi na askari wakafanikiwa kujeruhi majambazi wanne na kufanikiwa kupata bunduki ya kijeshi aina ya SMG iliyofutwa namba za usajili ikiwa na risasi 22 ndani ya Magazine" Amesema Siro.
Amesema kuwa majeruhi hao walikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili na wakati wanapatiwa matibabu wote kwa bahati mbaya walifariki Dunia kutokana na majeraha ya risasi.
Ameongeza kuwa uchunguzi huo umebaini kuwa Bunduki hiyo ni moja ya zile zilizoporwa wakati askari wakibadilishana lindo.