Kwa msaada wa Daily Mail.
Borussia Dortmund 2-1 Real Madrid – Champions League Kundi D, October 2012
Hii ilikuwa mara ya kwanza wanakutana ambapo ilishuhudia Klopp akiwa na klabu yake ya Borrusia Dortmund wakiibuka wababe dhidi ya Mourinho na Real Madrid.
Robert Lewandowski alifunga bao la kwanza lakini mchezaji bora wa Ulaya kwa sasa Cristiano Ronaldo alisawazisha ndani ya dakika mbili tu, Marcel Schmelzer alimaliza kazi kwa kufunga bao dakika ya 64 ambalo lilifunga hesabu. Ushindi huu uliipeleka Dortmund kileleni mwa kundi hilo.
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Subotic, Hummels, Piszczek, Schmelzer, Kehl, Bender (Gundogan 67), Gotze (Schieber 87), Reus (Perisic 90+1), Grosskreutz, Lewandowski
Real Madrid: Casillas, Varane, Essien, Pepe, Ramos; Khedira (Modric 20), Alonso, Ozil, Di Maria, Ronaldo, Benzema (Higuain 73)
Real Madrid 2-2 Borussia Dortmund – Champions League Kundi D, November 2012
Mchezo wa pili ulifuata mwezi Novemba ambapo ulichezwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Katika mchezo huu ulimalizika kwa sare lakini ilikuwa ni madrid ambao walisawazisha mara mbili mfululizo.
Marco Reus, alifunga goli la kuongoza kabla ya mchezaji mtata Pepe hajasawazisha kwa upande wa Madrid. Alvaro Arbeloa alijifunga na kuipa uongozi Dortmund lakini mchezaji Mesut Ozil equalised akasawazisha mchezo ukielekea mwisho.
Real Madrid: Casillas, Ramos, Varane, Pepe, Arbeloa (Kaka 78), Xabi Alonso, Modric (Essien 46), Di Maria, Ozil, Ronaldo, Higuain (Callejon 46)
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer, Gundogan (Perisic 81), Kehl, Reus (Bender 74), Gotze (Leitner 90+1), Grosskreutz, Lewandowski
Borussia Dortmund 4-1 Real Madrid – Champions League Nusu Fainali ya kwanza, April 2013
Fainali ya mwaka 2013 ilikuwa ichezwe kwenye uwanja wa Wembley na nusu fainali iliwakutanisha wababe hawa tena, moja ya mechi zitazakokumbukwa sana. Huu ulikuwa mchezo uliowastua watu wengi hasa ukizingatia ilikuwa ni Madrid ambayo weni walitarajia Mourinho asifanye kosa.
Robert Lewandowski alifanya moja ya vitu vyake hatari zaidi uwanjani akiinyanyasa Madrid kwa kufunga magoli manne katika ushindi wa Dortmund wa 4-1 dhidi ya vijana wa Jose Mourinho yaani Madrid.
Lewandowski alimpa Mourinho kipigo kikubwa zaidi kocha huyu kuwahi kukipata katika michezo yake 106 ya Uefa Champions League.
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek (Grosskreutz 83), Subotic, Hummels, Schmelzer, Bender, Gundogan (Schieber 90), Blaszczykowski (Kehl 82), Gotze, Reus, Lewandowski
Real Madrid: Diego Lopez, Sergio Ramos, Varane, Pepe, Fabio Coentrao, Khedira, Alonso (Kaka 80), Ozil, Modric (Di Maria 68), Ronaldo, Higuain (Benzema 68)
Real Madrid 2-0 Borussia Dortmund – Champions League Nusu Fainali ya Pili, April 2013
Madrid walikuwa wakutegemea kugeuza matokeo baada ya kupigwa 4-1 katika mchezo wa kwanza, na walicheza mchezo huo kwa kasi ya kipekee.
Lakini Dortmund hikuwa nyepesi kupenyeka mpaka katika dakika 10 za mwisho ndipo ambapo Madrid walipata mabao yao mawili.
Karim Benzema alifunga bao la kwanza dakika ya 82 kabla ya Ramos kufunga dakika ya 88.
Real Madrid: Diego Lopez, Essien, Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao (Kaka 57), Modric, Alonso (Khedira 67), Di Maria, Ozil, Ronaldo, Higuain
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer, Gundogan, Bender (Felipe Santana 90), Blaszczykowski, Gotze (Grosskreutz 14), Reus, Lewandowski (Kehl 87)
Chelsea 1-3 Liverpool – Premier League, October 2015
Klopp alikuwa akiiongoza klabu yake mpya ya Liverpool katika mchezo wake wa tatu tu tangu aichukue timu kutoka mikononi mwa kocha Brendan Rodgers ambaye alikuwa ametimuliwa.
Akiwa ametoka kupata sara dhidi ya Tottenham na Southampton, Klopp akawa anaelekea Stamford Bridge kwa ajili ya kuendelea kusaka ushindi kwa ajili ya klabu yake mpya.
Mara hii pia Klopp aliweza kumchapa Mourinho kwa bao tatu kwa moja.
Coutinho akiwa katika kiwango bora alifunga mabao mawili huku pia Benteke akiongeza la tatu ikiwa ni baada ya Ramires kuipa Chelsea bao la kuongoza.
Chelsea: Begovic ; Zouma, Cahill, Terry, Azpilicueta (Falcao 75); Ramires, Mikel (Fabregas 69), Willian; Oscar, Hazard (Kenedy 59), Costa
Liverpool: Mignolet; Clyne, Skrtel, Sakho, Moreno; Can, Lucas, Milner(Benteke 64); Lallana (Lovren 90), Coutinho, Firmino (Ibe 75)
Tarehe 17/10 yaani Jumatatu itakuwa ni Liverpool dhidi ya Manchester United… Nani ataibuka mbabe, ni Klopp au ni Mourinho?