SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 13 Oktoba 2016

T media news

ALI KIBA ADAI SINGELI NI MZIKI MZURI SANA ILA UNAKOSA STAHA, PIA AFUNGUKA KUHUSU ‘AJE REMIX’

Kiba amesema ni shabiki na mpenzi mkubwa wa mziki wa singeli lakini maneno na lugha wanazotumia katika nyimbo hizo zinamfanya asiufurahie mziki huo.Kiba ameiambia Planetbongo kuwa mziki wa singeli kwa sasa unapendwa sana kwa hiyo ni wakati wa wasanii wake kutumia maneno yanayoweza kutumika katika maongezi ya kawaida.
Anasema licha ya kuupenda lakini huwa hasikilizi sana kwa kuhofia kumuathiri katika uandishi wake naye akajikuta anaandika maneno hayo ya wanasingeli ambayo ni lugha zisizokuwa na staha inayotakiwa.

AJE REMIX INAKUJA..
Kiba pia ameweka wazi kuwa video ya aje remix imeshakamilika ambayo wameifanya na rapa mnigeria M.I, lakini kiba amesema, ilibidi waongeze baadhi ya vionjo kwenye wimbo ili kuutofautisha na ule uliovuja.Amedokeza video ina kucheza kwingi na anaonekana msichana mmoja tu na alikiba Kwenye video hiyo.
Aje ya AliKiba anayoitoa kama remix ndiyo ilikua toleo original lakini ikavuja kabla ya kutoka rasmi.