Ni wakati muafaka sasa vyama vyetu vya siasa vinavyojiita ni vya upinzani vijipime kama vinatosha kua vyama vya upinzani ama ni upinzani uchwara?
Vyama hivi ambavyo ndani yake haviishi migogoro na misukosuko,ambayo inaashiria ukandamizwaji na uminywaji wa demokrasia ndani yake leo vinatuaminisha utawala uliopo ni wa kidikteta..
Nani hakumbuki sakata la Zitto alivyodhubutu kutangaza kugombea urais kupitia chama chake cha Chadema,na baadae anatafutiwa zengwe na kufukuzwa chamani,leo hata yeye mwenyewe ameusahau Udikteta aliofanyiwa enzi zile na anaunga mkono harakati za Chadema kutuaminisha Magufuli ni Dikteta.
Nani hakumbuki kilichomkuta Dr. Slaa, au nani hakumbuki upinzani wa Dr. Slaa, ulikua ni upinzani imara wenye masilahi mapana kwa taifa letu,lakini Dr. Slaa alivopinga kuja kwa Lowassa chamani akaambiwa ni bora yeye aondoke ili Lowassa apate nafasi.
Chama kinaendeshwa na maamzi ya mtu mmoja mbona sisi wanachama hatukushirishwa kwenye mchakato wa kumpokea Lowassa ama kumkataa, na sisi ni wanachama? Si kweli kwamba kila mwanachama wa chadema alifurahishwa na kitendo hicho, chama kinaongozwa kama familia yenye mfumo dume.
Nani pia hakumbuki jinsi mchakato wa kumpata katibu mkuu wa sasa wa chama chetu?,mchakato uligubikww na mizengwe kibao,ilimradi tu mwenyekiti anaamua nani akae kwenye nafasi hiyo, na kwa nn mwenyekiti kang'ang'ania madaraka? Chama hakina utamaduni wa kuachiana uongozi?..hayo yote na mengine yanaonesha wazi upinzani wa Chadema ni Upinzani Uchwara, M/kiti anakanyaga katiba ya chama hivi leo akiingia ikulu atashindwa kukanyaga katiba ya nchi?
Nani hakumbuki kua hichi chama ndo chama kilichoanzisha vuguvugu la ufisadi pale bungeni miaka kadhaa iliyopita na waziwazi wakatuaminisha kua Lowassa ni mtuhumiwa namba moja wa Ufisadi,leo wanakuja na ngojera za kutuaminisha Lowassa ni mtukufu kwa kua wamekalia hizo nyaraka za ushahidi...hivi hapa napo panahitaji usomi kiasi gani kujua hawa ni wapinzani uchwara? Maana sio Slaa,sio Tundu Lissu, sio Peter Msigwa, sio Mnyika,na wala si Mbowe wote walimtuhumu Lowassa.
Kwa majirani zetu na penyewe kumenuka,Lipumba alijiuzuru tena kwa mbwembwe, kwa kuitisha press leo anatangaza yeye ndo mwenyekiti halali wa chama,kwani hivi vyama havina katiba? Sasa kama nyie wenyewe ni madikteta kwenye vyama vyenu, huo mnaotuaminisha ni udikteta uchwara mtaweza kupambana nao?
Ifike pahala watanzania tuamue kutokuwaunga mkono nyie upinzani uchwara, kama miaka kadhaa mlituaminisha kua Tanzania inahitaji rais mwenye maamuzi,rais asie chekacheka mwenye kusimama hadharani na kukemea ufisadi na ubadhairifu wa mali za umma, Mungu si kiziwi kasikia maombi yenu katupa kiongozi ambaye leo tuna sababu lukuki za kujivunia,kiongozi ambaye hajamaliza hata mwaka lakini tayari tumeshaona dira na mwelekeo wa wapi tunaenda.
Cha ajabu kila anachokifanya kizuri kwa watanzania nyie kwenu ni kuponda tu, hivi ni kweli hamuoni,Majipu yaliyotumbuliwa,hamuoni elimu bure?,hamuoni pesa zilizookolewa kupitia watumishi hewa?,hamuoni pesa zilizookolewa kwa kudhibiti ukusanyaji kodi?,hamuoni pesa zilizookolewa kwa kufutwa kwa maazimisho ya siku kuu za uhuru na muungano?,hamuoni ni sh ngapi zimeokolewa kwa kuzuia safari za nje?,hamuoni hata jitihada za serikali kubadili mfumo wa elimu ambao ulikia umechakaa?,hamuoni hata madawati? Mnachoona ni Udikteta uchwara..
Hivi ukuta utatumia sh ngapi? Kwa nini hiyo bajeti msiielekeze kutatua kero za wananchi kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na serikali? Kama kweli mna uchungu na sisi(watanzani) leo hii huu ukuta unamfaishaje mkulima,mama ntilie?mwanafunzi?wazee?,na watanzania wa kawaida hata wafanyabiashara,....lakini huo mnaouita udikteta uchwara ukimuuliza mtanzania wa kawaida atakuambia amepata elimu bure,shirika la ndege limefufuliwa,bomba la mafuta kutoka Uganda linajengwa ambalo litareta ajira na kukuza uchumi,reli itajengwa ndani ya miaka mitatu,elimu bure nk..
By Mashibes/JF