Ni kawaida kukuta maisha wanayoishi Wanasiasa ni tofauti na wapiga kura wao lakini sio hivyo kwa Rais wa Uruguay ambae anaishi kwenye maeneo ya mashambani na anatoa sehemu kubwa ya kipato chake kusaidia watu masikini.
Umri wa Jose Mujica ni miaka 78 ambapo May 20 mwaka huu anatimiza miaka 79
1. Yani nguo zake zinafuliwa kawaida na kuanikwa nje tu, pia maji anayotumia ni ya kisima ambacho kina magugu mengi.
2. Analindwa na Polisi wawili na mbwa na aliikataa kukaa kwenye nyumba ya serikali aliyopewa na badala yake kaenda kuishi kwenye nyumba ya mke wake huko mashambani ambako kuna mazingira ya kimasikini sana ikiwemo barabara mbovu nje kidogo ya mji wa Montevideo.
3. Rais na mkewe hufanya kazi ya kuotesha maua wao wenyewe yakiwa ni maisha ya kipekee kusikia ni ya Rais wa nchi.
4. Mujica anatoa asilimia tisini 90% ya mshahara wake wa kila mwezi kusaidia watu masikini huku akisema ‘naweza kuonekana kama mzee wa jadi lakini maisha haya nimeyachagua mwenyewe, naweza kuishi vizuri na kile nilichonacho.
5. Rais huyu kwa mwezi matumizi yake hayazidi shilingi milioni moja laki nne za Kitanzania ambapo kwenye kuorodhesha kiwango cha kipato cha kila kiongozi kwa mwaka na mali binafsi ikiwa ni lazima nchini humo kwa viongozi mbalimbali wa serikali mwaka 2010, alikutwa na kiasi cha dollar $ 1,800 tu kiasi ambacho hakizidi shilingi milioni tatu za kitanzania.
6. Gari anayotumia ndio hiyo picha ya kwanza hapo juu ambayo ni ya mwaka 1987 aina ya Volkswagen Beetle.
7. Mujica aliwahi kupigwa risasi mara sita na alitumikia kifungo miaka 14 jela ambapo muda wake mwingi kizuizini alikua katika mazingira magumu na kutengwa, mpaka alipoachiliwa huru mwaka 1985 wakati Uruguay ilivyorudi kwenye demokrasia.
8. Akiwa jela Mujica anasema hali ile ilimbadilishia mtazamo wake juu ya maisha na anakwambia ‘mimi naitwa rais maskini lakini mimi wala sihisi umaskini wowote, watu masikini ni wale ambao kazi yao ni kuishi maisha ya gharama ambayo inawasababisha kufanya kazi sana ili waendelee na maisha ya gahrama na kupata zaidi’
Mujica aliwalaumu viongozi wengi wa dunia ya kuwa na “upofu wa kutaka kukua na matumizi, kiasi kwamba isipokua hivyo itakuwa mwisho wa dunia.