SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 21 Septemba 2016

T media news

RC Lindi asimamisha kazi watumishi wanne

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi amewasimamisha kazi watumishi wa nne wa idara ya ardhi akiwemo afisa mipango miji wa mkoa huo kutokana na tuhuma mbalimbali za kuhusika katika migogoro ya ardhi.

Mhe. Godfrey Zambi amechukua hatua hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika mkoa wake katika maeneo mbalimbali ikiwemo na ujenzi wa barabara zinazoendelea kujengwa mkoani humo.

Mbali na afisa mipango miji huyo Hamidu Mtemekela, watumishi wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mikidadi Mohammed, Manase John na Raymond Cholobi.

Katika hatua nyingine katika ziara hiyo mkuu wa mkoa huyo aliwataka wakandarasi waliopewa zabuni za kujenga barabara mkoani humo wamalize kwa muda uliopangwa.